APP sensor (Accelerator Pedal Position Sensor)

Accelator Position Sensor, au ‘sensa’ ya kanyagio cha kuongeza kasi ya gari, namna jina ilivyo, inapeleka umbea kuhusu kiwango dereva amakanyaga ki kanyagio, kwenda kwenye kompyuta ya gari!

Sasa, kulingana na habari hii, kompyuta itajua niaje kuhusu kiasi cha mafuta cha mafuta uachiliwa kuchomwa, obviously na kiasi gani cha hewa ile throttle iwachilie!
Sensoryenyewe ipo hapo, juu ya kanyagio!


Moduli ya kanyagio inaweza kuundwa kwa uchawi wa, potentiometer au wa Magnetic Hall Effect, kulingana, au namna hii video itakuonesha ndani zaidi!

Namna yeyote, lakini Sensor hii inasajili fasta fasta harakati na msimamo wa kanyagio cha kuongeza kasi.


May be ukitaka ‘kulewa’ zaidi sana kuhusu huo uchawi wa Magnetic Hall Effect, bonyeza tu HAPA au kwenye hii picha chini!

Jinsi umeelewa, au kukumbuka, hii sensor inapeleka umbea kwenye kompyuta ya gari, alafu kompyuta inamuambia Throtle kiasi ya kufunguka, obviously na blaa bla zingine kwenye CAN, kiasi cha mafuta kinachohitajika, kulingana…
Na sababu kwanini zinakuanga sensor mbili ndani ya moja, au?

Sawa, jinsi tumejua kompyuta au ECU inatuma umeme 5V kuzungukia kwenye kila moja ya hizi sensor nani ya APP sensor, na juu ya huo uchawi wa  Hall Effect au Variable Resistance, kulingana kiasi ya mzunguko ata resistance itabadilika!
Sasa, wakati unapima, ukiona waya 6, lazima upate 5V mbili, ground au negative mbili, na siginal ….mbi?