Siku hizi almost kila kitu kinaundwa kuwa na hii blaa bla ya CONTROL SYSTEMS, mfano, AC za ofisini, nyumbani mataa yanajiwasha yenyewe, gari za siku hizi kila kitu mafundi wanazungumza ‘kontulo’ yaani control (ECU) ama kompyuta ya gari, nk!
Hapa tunaelezana kwa ufupi, maana na jinsi, au namna huu uchawi wa CONTROL SYSTEM unakuwa!
Imagine huu mfumo wa hesabu
X + 5 = Y
(5 haibadiriki, lakini X au na Y inaeza kuwa chechote)!
X ikiwa 2, ina maana Y itakuwa 7
2 + 5 = 7
Ina maana ukitaka mfumo wako uwe tu wenye 7 kama matokeo, lazima X uingize iwe 2, au na vinginevyo! Ukitaka matokeo au Y iwe 9, hapo lazima X iongezeke kuwa 4!
Tayari, hapa 5 ni control!
Huo mfumo 5 (control) kudhibiti matokeo kwenye Y(output) kulingana X (input) itakachokuwa, ni CONTROL SYSTEM wa X + 5 = Y
CONTROL SYSTEM ni mfumo ambao matokeo yanategemea maingizo!Kwa mfano wetu pale juu,
Input ni X, Control ni 5, alafu Output ni Y!
Alafu hizi CONTROL SYSTEMS zinaundwa kwa aina au namna mbili! Kuna zile ambao hamna aja ya kuthibitisha au ku comfirm matokeo, a.k.a OPEN LOOP CONTROL SYSTEMS, alafu na zile ambao lazima, au ata matokeo yanafanya uchawi ata kwenye mainginzo, ambao ni CLOSED LOOP CONTROL SYSTEM!
Naomba, ili kueleezana viruzi tofauti kati ya hizi aina, kutumisa mfano wa ile AC ya kudhibiti ujoto chumbani au ata ikiwa gari!
OPEN LOOP CONTROL SYSTEM
Imagine, hiyo siginal ya INPUT inatokea kwenye Temperature sensor inaochunguza ujoto chumbani au ata kwenye gari, mfumo ni kwamba hiyo Temperature sensor ikipeleka umbea kwamba kuna ujoto chumbani, hapo AC itaanza, yaani itawaka tu, hata kama hakuna mtu yeyote chumbani! Sasa ndo hizi OPEN LOOP CONTROL SYSTEM!
CLOSED LOOP CONTROL SYSTEM
Sasa hiyo siginal ya INPUT inatokea kwenye Temperature sensor imeruhusu AC kuanza, lakini AC ikiwaka lazima kuna ijulishe au ipeleke umbea kwamba nimewaka! Sasa huko sehemu ndo kuna blaa blla zingine kuchunguza kama kuna watu au la, ikiwa la AC itajizima yenyewe! Huo mzunguko ndo CLOSED LOOP CONTROL SYSTEM!
Kukitokea mfano tatizo, tuseme huku AC inawaka hata bila watu au vinginevyo, ukifanya diagnosis hizo blaa blaa za OPEN LOOP detected!