Engine Control Unit, a.k.a ECU, yaani kompyuta ya injini, ni kitengo cha kudhibiti injini (ECU), au tuseme ni kifaa kinachodhibiti mifumo mingi ya injini katika kitengo kimoja, pia huitwa moduli ya kudhibiti injini (ECM)!
Tafadhali, niruhusu niweke blaa bla hii katika hali ya jinsi ilivyokuwa! Ikiwa unataka ile ilirekebishwa, kwa lugha yetu ya asili, bonyezaHAPAΒ π
Resistors, yaaani Rizisita, zinazuia mtiririko wa umeme!
Uzuiaji huu unaweza kuja na manufaa katika hali nyingi, especially katika vifaa vya umeme!
Hii πvideo inaelekezea kila kitu, kuanzia kwa jinsi hizi rizisita hizi zinavyofanya kazi, jinsi au wapi zinatumiwa, ikiwa ni pamoja na jinsi zinazyopangwa na kupimwa kukiwepo matatizo yoyote!
Jinsi umeona, kila rangi iliopo kwenye resistor ina maana!
ππππππ BONYEZA HAPA
ku caliculate hizo color codes!
Accelator Position Sensor, au ‘sensa’ ya kanyagio cha kuongeza kasi ya gari, namna jina ilivyo, inapeleka umbea kuhusu kiwango dereva amakanyaga ki kanyagio, kwenda kwenye kompyuta ya gari! Sasa, kulingana na habari hii, kompyuta itajua niaje kuhusu kiasi cha mafuta cha mafuta uachiliwa kuchomwa, obviously na kiasi gani cha hewa ile throttle iwachilie!
Sensoryenyewe ipo hapo, juu ya kanyagio!
Moduli ya kanyagio inaweza kuundwa kwa uchawi wa, potentiometer au wa Magnetic Hall Effect, kulingana, au namna hii video itakuonesha ndani zaidi! Namna yeyote, lakini Sensor hii inasajili fasta fasta harakati na msimamo wa kanyagio cha kuongeza kasi.
May be ukitaka ‘kulewa’ zaidi sana kuhusu huo uchawi wa Magnetic Hall Effect, bonyeza tu HAPA au kwenye hii picha chini!
Jinsi umeelewa, au kukumbuka, hii sensor inapeleka umbea kwenye kompyuta ya gari, alafu kompyuta inamuambia Throtle kiasi ya kufunguka, obviously na blaa bla zingine kwenye CAN, kiasi cha mafuta kinachohitajika, kulingana… Na sababu kwanini zinakuanga sensor mbili ndani ya moja, au?
Sawa, jinsi tumejua kompyuta au ECU inatuma umeme 5V kuzungukia kwenye kila moja ya hizi sensor nani ya APP sensor, na juu ya huo uchawi w
a Hall Effect au Variable Resistance, kulingana kiasi ya mzunguko ata resistance itabadilika!
Sasa, wakati unapima, ukiona waya 6, lazima upate 5V mbili, ground au negative mbili, na siginal ….mbi?
MAP sensor, au, Manifold Absolute Pressure Sensor, inapima kiasi au uzito wa mkusanyiko wa hewa uliopo kwenye ‘intake manifold’!
Mkusanyo wa hewa ukijumulisha na hewa inaotoka njia za mfumo zingine kama, EGR, TURBO, PCV, nk!Manifold ni hicho ki bla blaa kabla hewa kuingia cylinder au baada ya Throttle
Hii sensor inaeza kuwekwa popote, kulingana gari, ili mradi kuna njia yakufikia kupima hiyo hewa!
Ukitaka maelekezo mengine ya ndani ndani, namna inavyofanya kazi wapi vipi, nk, unaeza kutazama hii video
May be ukitaka kuelewa zaidi kuhusu huo uchawi wa Piezo ambao Pressure sensor nyingi zinategemea, bonyeza HAPA kwenye hii link au picha hapa chine LINK
Sensor hiyo mara nyingi inaka namna hii
Jinsi yalivyoelezwa yote kwenye hizo video, sensor hii inaweza kuwa na waya tatu au waya nne.
Mara nyingi reference voltage inakuwaga 5V kutoka kwenye ECU!
Jina kamili la hii Sensor ni, Mass Air Flow Sensor! Kwa wengi inajulikana zaidi kama MAF sensor, mara Air Mass, nk! Ingawa inaweza kuwa na majina mengi, inawajibika kwa kazi moja tu, kupima kiasi cha hewa, na ujoto wa hiyo hewa, inayoingia kwenye injini, na kupeleka taarifa hii kwenye kompyuta ya gari, yaani ECU au PCM au ‘kontulo boxi’! Kompyuta au ECU kulingfana hii taarifa, ndo itajua kiasi gani cha mafuta kinachohitajika!
Hii sensor imewekwa kwenye bomba la uingizaji hewa, baada ya chujio au filter ya kusafisha hewa! Hapo chini kuna video inaonesha kila so tunafanya maandishi haya kuwa mafupi, chini kwenye hii page tunakupa muhtasari mafupi au summary, ikiwa ungependa maelezo zaidi, unaweza kutazama video! Kwenye video kuna blaa blaa ya aina za hii sensor!
HAPA NDO VIDEO UKITAKA KUTAZAMA ULEWE ZAIDI
Nadhani umehelewa kwanini zingine utakuta zina waya moja, mbili, zingine tatu, zingine nne, tano, sita, nk! Zikwa waya tatu au nne inakuwa tu Air flow meter ya kupima tu uzito!
Ikiwa way moja au mbili inakuwa tu Intake Air Temperature ya kupima tu ujoto wa hewa inaoingia! ECU inatuma 5V zizungunkie kwenye hii sensor, kulingana mbadiliko ya resistance, hapo ECU iatajua kama ni mazingira ya baridi au moto!
Na zikiwa tano au ata sita, kumanisha Airflow Meter pamoja na Intake Air Temperature, au Mass AirFlow SensorECU inatuma +5V na -5V zizungukie kwenye upande wa IAT katika hii sensor! MAF power (+) inatokea battery moja kwa moja ikiwa switch ON! Ground ya MAF inakuwa ya kugawana! MAF siginal ndo inaenda kwa ECU, Negative au Ground ya siginal inapatikana automatically, hahahahahhah…
Lakini, kwenye mfimo mingine, unaezakuta hakuna upande wa IAT sensor, inakuwa upande wa kupima uzito tu! Waya zote nne zinakuwa niaje kama hapa chini!
Au kugawana waya moja GROUND, lakini kila kitatoka kwenye ECU
Siku hizi almost kila kitu kinaundwa kuwa na hii blaa bla ya CONTROL SYSTEMS, mfano, AC za ofisini, nyumbani mataa yanajiwasha yenyewe, gari za siku hizi kila kitu mafundi wanazungumza ‘kontulo’ yaani control (ECU) ama kompyuta ya gari, nk!
Hapa tunaelezana kwa ufupi, maana na jinsi, au namna huu uchawi wa CONTROL SYSTEM unakuwa!
Imagine huu mfumo wa hesabu
X + 5 = Y
(5 haibadiriki, lakini X au na Y inaeza kuwa chechote)! X ikiwa 2, ina maana Y itakuwa 7 2 + 5 = 7 Ina maana ukitaka mfumo wako uwe tu wenye 7 kama matokeo, lazima X uingize iwe 2, au na vinginevyo! Ukitaka matokeo au Y iwe 9, hapo lazima X iongezeke kuwa 4!
Tayari, hapa 5 ni control!
Huo mfumo 5 (control) kudhibiti matokeo kwenye Y(output) kulingana X (input) itakachokuwa, ni CONTROL SYSTEM wa X + 5 = Y
CONTROL SYSTEM ni mfumo ambao matokeo yanategemea maingizo!Kwa mfano wetu pale juu, InputΒ ni X, Control ni 5, alafu Output ni Y!
Alafu hizi CONTROL SYSTEMS zinaundwa kwa aina au namna mbili! Kuna zile ambao hamna aja ya kuthibitisha au ku comfirm matokeo, a.k.a OPEN LOOP CONTROL SYSTEMS, alafu na zile ambao lazima, au ata matokeo yanafanya uchawi ata kwenye mainginzo, ambao ni CLOSED LOOP CONTROL SYSTEM!
Naomba, ili kueleezana viruzi tofauti kati ya hizi aina, kutumisa mfano wa ile AC ya kudhibiti ujoto chumbani au ata ikiwa gari!
OPEN LOOP CONTROL SYSTEM
Imagine, hiyo siginal ya INPUT inatokea kwenye Temperature sensor inaochunguza ujoto chumbani au ata kwenye gari, mfumo ni kwamba hiyo Temperature sensor ikipeleka umbea kwamba kuna ujoto chumbani, hapo AC itaanza, yaani itawaka tu, hata kama hakuna mtu yeyote chumbani! Sasa ndo hizi OPEN LOOP CONTROL SYSTEM!
CLOSED LOOP CONTROL SYSTEM
Sasa hiyo siginal ya INPUT inatokea kwenye Temperature sensor imeruhusu AC kuanza, lakini AC ikiwaka lazima kuna ijulishe au ipeleke umbea kwamba nimewaka! Sasa huko sehemu ndo kuna blaa blla zingine kuchunguza kama kuna watu au la, ikiwa la AC itajizima yenyewe! Huo mzunguko ndo CLOSED LOOP CONTROL SYSTEM!
Kukitokea mfano tatizo, tuseme huku AC inawaka hata bila watu au vinginevyo, ukifanya diagnosis hizo blaa blaa za OPEN LOOP detected!
This is complete factory service repair workshop manual has easy-to-read text sections with top quality diagrams and instructions.
They are specifically written for the do-it-yourselfer as well as the experienced mechanic. With step by step instruction & highly detailed exploded pictures & diagrams to show you how to complete the required job correctly & efficiently .
Provides step-by-step instructions based on the complete dis-assembly of any system or parts. Yes, it is this level of detail, along with hundreds of photos and illustrations, that guide You through each service and repair procedure.
This Factory Service Manual generally covers General Information, Service Information, Suspension, Driveline, Brakes, Steering, Engine Mechanical, Cooling, Starting, Ignition, Emission Controls, Engine Controls, Transmission, Transaxle, Exhaust System, Fuel System, HVAC, Instrumentation & Warning Systems, Battery & Charging System, Audio Systems, Lighting, Electrical, Body Interior – Exterior and more…
This video previews of the contents, covering RangeRover, Discovery, Freelander, Defender
Tulijaribu kuelekezana kuhusu data ya kwenye IC/EEPROM/CHIP, as in, namna ya kusoma, edit, delete, copy, nk hizo EEPROM data! Kama bado hujapitia, na unataka kupata idea ya niaje hizo blaa blaa, then bonyeza hapaπ www.5021.tips/ujanja/eepromwork π
Sasa unaeza kuwa huna mashine yeyote ya hizo EEPROM na kweli unataka kufanya mazoeziπ€·ββοΈ!Β So what we have done, ni kuwekea hapa software inasoma hizo data, pamoja na mfano ya hizo EEPROM data ili ufanye mazoezi ku edit, delete, blaaa blaaa, you know?
SOFTWARE YA KWANZA na maelekezo ya matumizi kwenye hii video kiisha download hapo chini ya hii video
Hata kama EARTH na GROUND ni kama kitu kimoja, lakini ni tofauti! Kwa kingereza ya Merikani wanasema GROUND, alafu kwa Kingereza ya Ulaya(Europe) ni EARTH, so sometimes maana inakuwa confused!Β So is why we tried to explain the difference in this video
This service manual iko kwa lugha ya English, and it has been prepared to provide SUZUKI service personnel with the necessary information and data for the correct maintenance and repair!
This manual includes the procedures for diagnosis, maintenance, disassembling, reassembling, inspection and adjustment of components and diagnostics for guidance of experienced mechanics.
This manual explains items specific to parts used in the TOYOTA AVENSIS Common Rail SystemΒ Construction and operation, supply pump blaaa blaaa OCV, nk!
The purpose of this section is to help you understand the general diagnostic process that you will follow regardless of the type of customer concern you are troubleshooting…..and also to know about the features of diagnostic tools that will help you with greater accuracy
and speed…..not forgeting the lay out the troubleshooting steps and resources you will need to follow when diagnosing customer concerns.
This book is intended to provide an in-depth introduction to the hardware and technology of the personal computer and to answer your questions about how it all works.
Everyday we are challenged with new technology and new adaptations of existing technology with the result that we are continually all beginners. While this book is written primarily for people who wish to know more about personal computer (PC) hardware, it may also prove to be helpful to people who wish to expand their knowledge of the PCβs hardware.
Sasa, this is intended for the technical personnel responsible for service and maintenance of MercedesBenz trucks.
The contents in here are split up into: β’ function descriptions β’ component descriptions β’ Description of location of electrical connectors, sockets and ground points
Especially kwenye hizo gari zenye haziina hii OBD socket mpya ya 16PIN, pamoja na kwamba diagnosis mashine za siku hizi zinakuanga na socket moja juu siku hizi gari zote ni zenye hiyo socket moja! Ina maana gari yenye socketi tofauti ikitokea huwezi kupima kwa mashine!
….so HAPA UJANJA tuπ¨βπ Za ABS ziko chini ya hii document
Hapa tunajaribu kufafananua au kuelezeana maana ya maneno fulani ya kitaaalamπ, ambao tunatumia katika maisha yetu ya kila siku, bila kujua maanaπ€! So,HAPA UJANJA tuπ¨βπ
ENGINE SPEED inamanisha mwendo engine inazunguka (a.k.a RPM) alafu VEHICLE SPEED ni mwendo wa gari zima au tuseme muzunguko wa tayari although sio! Hizi sigina zinakuwa programmed tofauti tofauti as shown in this nonsense video!
Nguvu za maginetiπ zikija karibu kwa wire au kifaa chechote kinachopitisha umeme na kwamba kuna umeme unaopitaπ€kwa hiki kifaa, kuna uchawi funi utakaotokea kusababisha/kuzalisha umeme namna tulivyolekezana kwa hii videoπ! Kwasabu kwa maneno sijui niekwelekezeaje na maneno ganiπ aiiise!
Electronic Stability Program (ESP) ama Electronic Stability Control (ESC), au tena Dynamic Stability Control (DSC), ni uchawi wa ku improve a computerised vehicle’s stability by detecting and reducing loss of traction (skidding). ESP baada ya ku detect any loss of steering control, kuna namna it applies the brakes kuifanya gari irudi where the driver intends to go bila kupagawa namna tulijaribu kuelezea!
Nguvu za ule moshi unaotoka kwa engine unatumika kuzungusha aina ya kama pampu fulani hivi, na wakati wakuzunguka hii pump inanyonya au kuvuta hewa kutoka nje ya gari ili kuongeza kiasi cha hewa engine inahitaji kufanya kazi vizuri namna tulijaribu kueleza humu! Na pia kuna hizo pressure sensors, temperature sensor, nkπ€·πΌββοΈ !
Jinsi unafahamu engine za diesel zinatoa’nga moshi kali wenye vichembe (particles)π, sasa kwa kutaka kuzuia hizi particles zisitoke nje ya gari kuharibu mazingira, kuna kidude fulani kinawekwa kwenye exhaust pipe ya gari ya diesel ili kushika hizi particles!
Baada ya hizi particles kushikwa zinachoma mpaka kupotea namna tulijabuπkumbushana!
AIRBAG system iko na sensa ya kuchunguza kutikisa, ina maaana gari ikitikisa gafla kupiita kiasi, hii sensa itapeleka umbea kwa ECU (control boxi)!
Sasa, ECU ikipata itapeleka moto (power) kwa defletor na kulipuwa AIRBAGΒ namna tulijaribu kuoneshana hapaπpamojaΒ na chakufanya iliΒ kutoa/kuziima hiyo taa ya AIRBAGπ¨βπ§
Watu wengi wamebadilisha mafuta (OIL) ya gari lao wenyewe au wamepeleka gari kwa garage kwa wataalamu! Sasa, kipengele muhimu kuhusu blaa blaa ya mafuta (OIL) ni kuchagua aina ya OIL sahihi pamoja na right quantityπ€! I swear, unahitaji kuzingatia nambari zilizo kwenye lebo ya mafuta (OIL) ya gari. Unaweza kuona kitu kama “10W30” au “5W20” na ukashangaa wanamaanisha nini hikiπππ€£πππ .
A Virtual Private Server (VPS) uses virtualization software to partition physical servers into multiple “virtual” serversβeach having the ability to run its own operating system and applications. VPS is not for everyone, but is quickly becoming the hosting preference of choice for advanced Web developers who require root access to the server to run their own software.
Huu uchawi wa PIZOELECTRIC EFFECT ni kwamba, ukigonga au kukandamiza kitu kiliotengenezwa kwa ile kemikali ya crystal blaa blaaππ€£π, hicho kitu kinaweza kuzaa umeme. TENA ukipitisha umeme katika hicho kitu, kitatemeka (to vibrate/shake or move)! So ni vice versa namna tulijaribu kuoneshana kwenye hii videoπ€·πΌββοΈ
Kwa kutaka kuongeza nguvu za magari, bila kutumisa mafuta mengi, pamoja na bila kuharibu mazingiraπ€, wataalamu waligundua namna ya kuchunguza mafuta na hewa inaoingia kwenye engine…pamoja na kuchunguza huo moshi unaotoka kwa engineπ ili husiharibu mazingira nje ya gari. So waliweka sensor za kuchunguza na kupeleka umbea kwenye ECU/control box (computer), alafu ndo computer iwaambie actuators kazi ya kufanya, kulinganaπ€·πΌββοΈ! Sasa, kwasababu engine ya gari inategemea mafuta na hewa ili kuweza kufanya kazi, ndo maana njia za mafuta na hewa pamoja na hewa chafu (moshi) waliweka hizo sensor na actutors! So we shall look at all the sensors on in each systems as ellaborated in this video
AIRFLOW METER SENSOR
Either hii sensor inapima tu ujoto, AU inapima ujoto pamoja na uzito wa hewa inaoingia ndo hapo inaitwa Mass Airflow meter sensor!
Ikiwa inapima tu ujoto inakuwa na wire 2 tu
Iiwa inapima ujoto na uzito wa hewa, inaweza kuwa naπ€,
> 5 wires (2 yakupima joto, 3 za kupima uzito)
>4 wires (ground au negative wire ya upande wa kupima joto iko pamoja na ya upande wa kupima uzito)
>3 wires hakuna upande wakupima ujoto, inapima tu uzito wa hewa!
Hewa ikifika kwenye inlet manifold itakutana hewa ingine inaotokea njia zingine kama Turbo, EGR, EVAP system, nk! Ina maana lazima au bora kuwepo namna ya kupima jumla ya hewa iliopo kwenye manifold kabla kuingia kwenye engineπ€ hapo ECU ama control ijue kiasi cha mafuta itafanya injector zitoeπ! So, hii MANIFOLD PRESSURE SENSOR ndo inapima jumla ya hewa iliopo kwenye inlet manifold! Hii sensor mara nyigi ni 3 wiresπ€, moja ni 12V au 5V, ingine ni Negative/ground, Ingine ni ya SignalHii sensor ilitengenezwa kwa uchwa waPIEZOELECTRIC EFFECT, ukibonyeza hapatulijaribu kuonesha maana ya huu uchawi
Otherwise nama hii sensor inafanya kazi na kupimwa ili kujua kama ina tatizo, tulijaribu kuineshana katika hii video
ACCELERATOR PEDAL POSITION SENSOR
Sii ujajua hizi gari za kisasa kile ki pedal ni cha umemeβ‘ tofauti kwa zile gari za zamani kulikuanga ka metal fulaniπSasa hii sensor ina sensor mbili kwa moja, because the other ni ya emegency kama upande moja ukiharibika, namna ya ufanyaji kazi na kupimwa in this videoπ
Baada ya kuganyaga kwenye accelerator pedal umbea unapelekwa kwa ECU (control box) ili ijue namna ya kunfungua hiki ki blaa blaa THROTTLE cha kuruhusu hewa ingie kwenye Engine! Hii ELECTRONIC THROTTLE CONTROL iko na kile kiko ka ulimi ya mtu hiivi kufungua na kufungaπ€·πΌββοΈ! Kuna mota (motor) ya kutembeza hiki ki ulimi!Β Na kuna sensor ya kuchunguza hiki ki ulimi kimefunguka kiasi ganiπ€!
Namna ya kupima AND ufanji kazi tazama hii videoπ
Bila kufunga mfuniko wa kwenye tenki la mafuta, inasababisha upepo wa nje kuingia au ata mafuta kupotea kwa nja ya upepo (Evaporation)π! Sasa, ili kuhakisha unafunga mfuniko wa tenki, kuna sensa iliwekwa ili kwamba usipofunga, kuna taa itaonesha kwenye instrument cluster au ata taa ya check-engine yenyewe…au kuna uchawi ECU inafanya kwenye gari ili isitembee vizuri mpaka ufunge huu mfunikoπ!
Jinsi unavyojuaπ, ukiweka kitu chochote kilivyo kama maji (liquid substance) kwenye kama dumu hivi, ukichezesha (shake) hiyo dumu, kuna pressure inatokea! Sasa, ata maafuta kwenye tenki la gari, kila gari ikitembea obviously inacheza so yale mafuta kuna uchawi unatokea kuyafanya kubadilika kuwa ya upepo na kuongeza pressure kwenye tenki, ndo maana kuna FUEL TANK PRESSURE SENSOR yakuchunguza kiasi cha pressure kwenye tenkiπ!
Hii sensor ilitengenezwa kwa uchwa waPIEZOELECTRIC EFFECT, ukibonyeza hapatulijaribu kuonesha maana ya huu uchawi, so na maana ina 3wiresπ€·πΌββοΈ
Wakati gari inatembea, inachezesa tenki na kufanya yale mafuta (kama maji) kubadilika au ku evaporate kuwa upepoπ€! Sasa, hii EVAP SYSTEM inaosaidia kufanya uchawi ili yale mafuta ya upepo yasichanganyike au yasiende kwenye njia ya mafuta ya maji! Hii EVAP SYSTEM iko na njia mbadala yakupitisha upepo kwenda kwenye manifold au nje ya gari kulinganaπ¨!
Kuna ile meter ya kuchunguza kiasi cha mafuta kwenye tenki (tank), kuna pump, kuna ka sieve ka kusfisha hayo mafuta, naπ€….jinsi tuanelekezana kwa hii videoπ!
FUEL PRESSURE REGULATOR
Zamani, kwenye mfumo wa mafuta ya gari kulikuwanga pipe ya kurudisha mafuta kwenye tenki yakibaki, sasa kwa hizi gari mpya kuna sensor yakuchunguza kiasi cha mafuta yanaohitajika NA ndo hayo mafuta yatakaporuhusiwa kutoka! Ndo sababu ingine kwanini unaona ka pipe moja kwenye tenki! Sasa, tulijaribu kumbushana uchawi kwenye FUEL PRESSURE REGULATORπ¨βπ§
Ukitoa mugu kwenye accelerator pedal (ile yakuongeza nguvu ya gari) ata ule mfuniko wa kuruhusu hewa ingie kwa engine unazibaπ€ ina maana engine ikikosa hewa itazimikaπ€·πΌββοΈ! Sasa uchawi wa IAC valve ni kufungua ka njia fulani ile hewa ipite kufika kwa engine ata ukitoa muuguπ au tuseme ukitoka kwa gari inaendelea kuaka!
Assuming kwamba unajua crankshaft au camshaft ni nini, sasa ili kuweza kujua muda gani wakati cylinder fulani inafanya kitu gani na inahitaji nini, hizi CAMSHAFT na CRANKSHAFT POSITION SENSOR kuna uchawi unaziwezesha kujua ipi niaje, na kupleka huu umbea kwenye computer ya gari namna tulijaribu kumbushana au kuoneshanaπ»
Jinsi unavyojua, kifaa chenye uwezo kutembeza umeme kinabadilika kulingana ujoto au ubaridiπ€! So computer ya gari inatuma umeme kuzunguka kwenye hii ENGINE COOLANT TEMPERATURE SENSOR , kuligana ujoto/ubaridi umeme (volts) zitazorudi kwa computer, either itapungua au kubaki niaje namana tulioneshanaπ¨βπ§
Hii KNOCK SENSOR ione kama microphone, inachukua au kusikilizia sauti ya engine na kupelekea ECU (control box) umbea! Sasa kuna sauti ya kawaida ya engine ambao ECU imezoea, so like mafuta + hewa yakichomwa kwa muda au mahali ambao sio sahihi ya kwamba sauti ya engine itabadilika, hapo ECU ikipata sauti tofauti ya engine kupitia hii KNOCK SENSOR itajua kuna uchawi wa engine knock (a.k.a detonation) umetokea!
Obviously unafahamu kwamba baada ya engine kuchoma mafuta + hewa kuna moshi unaotokeaπ€, sii unajua au unaona huo moshini chafu, lakini huu moshi unafanywa kuzunguka kurudi au kuungana na ile hewa safi inaotokea nje gari! Sasa, huu moshi kufanywa kuzunguka na kurudi kwenye engine kuna uchawi mwingi unatokea, kama kushusha temperature ya engine, kupunguza moshi unaotoka nje ya gari ili usiharibu mazingira, na blaa blaa blaa zingine! Sasa hii EGR system unakuta kuna sensor & actuator nyigi ambao unapswa kujua au kumbukaπ¨βπ§!
Jinsi unafahamu, engine inahitaji mafuta & hewa ili vichanganyike vichomwe ndo engine ipata nguvuπ, ndiyo lakini kuna namna hewa & mafuta yanapaswa kuchanganyikwa (a.k.a stoichiometric ratio) as in kukiwepo mafuta lita 1 lazima hewa iwe kama lita 15π€·πΌββοΈ! Sasa, kukitokea na pamoja kuzuia uchawi kama mafuta yanakuja mengi au madogo, kuna hizi OXYGEN SENSOR ambao zinachunguza moshi unaotokea baada ya mafuta + hewa kuchomwa, so huu umbea unahusiana kuhusu hizo OXYGEN SENSOR, ziko wapi, zinafanyaje kazi, kupima nini, na blaa blaa zingineπ!
Sii unajua ufanyaji kazi wa engine, piston inanyonya hewa+mafuta alafu inagandamiza (compress) then blaa blaa kuchomaπ§, sasa kwenye kugandamiza (compress) kuna hewa + mafuta ina bypass kati ya piston na cylinder wall kujikuta kwenye sump (dumu ya oil chini ya engine)! Sasa kutoa hii hewa kuna ka pipe kanawekwa ili kunyonya huu upepepo as we tried show in hereπ¬
Kwenye AUTO TRANSMISSION, uchawi zaidi zaidi ni wa valve ambao valve zinategemea solenoid, zingine ni pressure sensor na temperature sensor! SO, kama ulihelewa vizuri kuhusu blaa blaa za hizi sensor kwenye system zingine, then ili muradi picha inakuonesha hii sensor iko wapi, then troubleshooting AUTOMATIC TRANSMISSION troubles ni kama kunywa majiπ»!
Uchawi kuweza blaa blaa ya ma sensor, control boxi, sijui actuators ni kujua mfano ni sensor gani, iko wapi, inafanya kazi gani, inafanyaje hiyo kazi as in iliundwaje (how it is made), nk! So ukipata umbea huu wote ndo utajua inahitaji kupeleka au kutoa umeme gani kutoka wapi au blaa blaa as we explained in hereπ¨πΌβπ !
Jinsi hii video inakuonesha, hiki kitabu kina namna ya ku program funguo za gari, mashine gani yakutumia, vifa gani vya kufungua/kufunga kwenye gari, nk! Yaani unapata almost kila umbea mhimuπ!
Technologia inabadilika kila sekunde, so ukiona mashine fulani ndo ilitumika, usikulupuke kununua hiyo mashine unaezakuta kuna mashine ingine mpya/bora! Hiki kitabu kikusadie tu kutoa mwanga kwa macho yako, nenda ufanye research nyingi zingine boraππΌ!
Kwanza moja kwa moja, ukumbuke how immobilizer systems work, what components involved, why and how to supercalifragilisticexpialidocious if lost or spare keysπ€·ββοΈ
Kwanzia hizo TRANSPONDER KEYS funguo za chuma za kawaida, mpaka hizo SMART KEY, tunaanza na mifumo, jinsi zinafanya kazi, ili uweze kuelewa kwanini, mashine fulani ndo zinazo kamilisha kazi fulani!
TRANSPONDER KEYS
Kwa kutaka kuzuia wizi, walifanya uchawi kwenye gari kwamba isipo kuwa funguo maalum ya hiyo gari maalum, hiyo gari haiwezi kuendeshwa. Kwenye funguo waliweka kadude fulani kanaitwa Transponder Sasa haka kadude namna tulivyoneshana kwa video, kuna neno siri ama PIN a.k.a password ambao lazima ifanane na ilyo kwenye gari. Isipo fanana gari haitawaka!
So, kwa hii video tulijaribu kuoneshana namna hiizi blaa blaa zote zinafanya kazi
Ina maana hiyo funguo maalum ya kuendesha gari maalum ikipotea lazima ufanye uchawi wa ziada kuirudisha namna tuliojaribu kumbushana katika hii video!
ONYOπ¨: Mara kwa mara kuna ujanja unaotokea wa nmna ya kufanya key programming, so hii ni just basics of what could be done in caseπ€·ββοΈ!
TRANSPONDER DETAILS
Na hata kama hizo transponder zinafanana kwa muonekano, lakini ziko tofauti kaaabisa! Yaani ziko na namba mf., ID46, 4C, TPX7, nk kulingana aina ya gari! Ina maana ukileta tranponder ya Toyota Corona kuiweka kwa system ya Toyota Carina, hazitafanyaπ€·πΌββοΈ namna tulioneshana kwenye hii video
Sasa kuna system zenye funguo za transpoder kama tumeone, na kuna smart key systems
SMART KEY SYSTEMS
Sasa, hizo smart zinabaki mfukoni kwamba unaeza kufungua mlango na kuendesha gari bila kuigusa hiyo funguo!
KEYLESS ama SAMRT KEY SYSTEM ina upande miwili, upande wa kuasha gari KEYLESS IGINITON SYSTEM, na upande mwingine wa tuseme kifahari hiiivi, KEYLESS ENTRY SYSTEM ile yakufungua mlango, booti, kutembeza viti, nk!
So namna hii video inakuonesha tutangaliza hizo part tofauti tofauti
KEYLESS IGINTION SYSTEM
Sasa tukianza na KEYLESS IGINTION SYSTEM tutaona namna SMART ECU ikishirikiana na ID CODE BOX, BODY ECU, ENGINE ECU, nk, kama TRANSMISION ECU, STEERING LOCK ECU, nk, ili kuwezesha engine kuaka kwa kutambua kama ndo funguo sahihi ilioko mfukoni ya huyo mtu anaejaribu kuendesha hiyo gari! Hii video ni ndeeefu pamoja na maneno mengi ya kurudia rudia ili uweze kuipata vizuri!
KEYLESS ENTRY SYSTEM
Sasa hapa tunajaribu kuoneshana KEYLESS ENTRY SYSTEM, utaona kwamba hapa ni SMART ECU na BODY ECU na componet zingine zinazohusiana…pamoja na uchawi gani unaweza kufanya kukitokea blaa blaa yeyote kwenye hii system!
Unajua kuna mashine nyigi na ni rahisi kutengeneza au kuongeza funguo ya smart. LAKINI ukikosea kidogo tu, ni hatari na kwamba system nzima utakuwa umehiharibuπ€·ββοΈ!
So be careful when diagnosising for problems or when using diagnosis machine as we tried ellaborate in this video
IMMO OFF & IMMOBILIZER DECODING
Kufanya IMMO OFF ni ule uchawi kufanya gari iwake na funguo yeyote kama kawaida au kama mifumo ya zamani.Β IMMOBILIZER DECODINGπ, ni kama ufunguo umepotea, unafuta kumbu kumbu ya ufunguo, kuirudisha kuwa bikira (virgin) kama mwanamke akiwa ajaolewa, namna gari inavyokuwa kiwandani!
Namna tulioneshana kwenye hii video, kufanya IMMO OFF either unaweka emulator au ku edit data za IC ama chip ya funguo!
ONYO π
kama unajelewa niaje, mambo ya EEPROM data blaa blaa, tumekuwekea hapa data za IMMO OFF na DUMPS (virgin Data), otherwise endelea kujifunza niaje!Β
Na, sometimes, ukiwa na secret codes fulani, ziwe SMART KEYS au TRANSPONDER KEYS, kwa kutumia ata diagnosis machine ya kawaida, unaweza kufanya ujanja fulani!Β So, tumekuwekea program kuwezesha kupata hizo secret codes fulani!
Tena tulijua kwamba funguo ikipotea unaweza kupata code/passsword kutoka hiyo EEPROM ili ukatumbukize kwenye funguo ingine ndo gari iwake, au pia kama control boxi imekufa unatoa haka EEPROM ukaweke kwa hiyo control boxi ingineπ!
Sasa uchawi ni kusipojua EEPROM ya funguo iko wapi na ni gani katika hizo nyingi zilizopo kwenye circuit board, maana iwe control boxi au immo box kuna EEPROM nyingi nyingi.
So hii Appπ² ya kwenye simu au na kompyutaπ», inakusadia kujua EEPROM ipi au Transpoder ipi inaendana hiyo gariπ€!
Sasa tayari umejua ni EEPROM gani ya funguoπ, je unajua nini chakufanya uweze kuisoma, kubadili ili ufanye IMMO OFF au DECODE ili kupata code/password ya funguo kutoka hiyo EEPROM?So ukibonyeza HAPA utona tulikumbushana au kuoneshana kuhusu data inakuanga humu, inakaje, inasomwa au kubadilishwa namna ganiπ€·πΌββοΈ hizo blaa blaa binary, HEX, address, nk, mara Flash Memory, EEPROM memory, nk!
Hiki kitabu kina namna ya ku program funguo za gari, mashine gani yakutumia, vifa gani vya kufungua/kufunga kwenye gari, nk!
Yaani unapata almost kila umbea mhimuπ! Ni PDFπ² popoteπ» kinafunguka!
Tuseme umepata idea ya namna funguo zinafanyaπ!
Na funguo ikipotea umejua kwamba unaweza kutumia data ya EEPROM kuweza kutenegeza ufunguo mwingine AU ukafanya IMMO OFF ukatoa tu immo system ili gari ikubali funguo yeyote.
Sasa changamoto ni kujua uchawi gani wa kufanya immo off au ku program funguo ingine kwa kutumia data ya EEPROM ndo maana ukitaka niajeπ’!
Tumekusanya kila aina ya programu, yaani software kufanya ujanja wowote kwenye kila gariπ€, bonyeza tu HAPA HAPA HAPAπ€·ββοΈ!
Huu ni mifano namna hizi softyware ziliopo! Ni nyiiingiπ!
Zamani, kwenye mfumo wa mafuta ya gari kulikuwanga pipe ya kurudisha mafuta kwenye tenki yakibaki, sasa kwa hizi gari mpya kuna sensor yakuchunguza kiasi cha mafuta yanaohitajika NA ndo hayo mafuta yatakaporuhusiwa kutoka! Ndo sababu ingine kwanini unaona ka pipe moja kwenye tenki! Sasa, tulijaribu kumbushana uchawi kwenye FUEL PRESSURE REGULATORπ¨βπ§
#FUELPRESSUREREGULATOR #AUTOMOTIVEFUELSYSTEM #5021tips