MAP sensor

MAP sensor, au, Manifold Absolute Pressure Sensor, inapima kiasi au uzito wa mkusanyiko wa hewa uliopo kwenye ‘intake manifold’!
Mkusanyo wa hewa ukijumulisha na hewa inaotoka njia za mfumo zingine kama, EGR, TURBO, PCV, nk!Manifold ni hicho ki bla blaa kabla hewa kuingia cylinder au baada ya Throttle

Hii sensor inaeza kuwekwa popote, kulingana gari, ili mradi kuna njia yakufikia kupima hiyo hewa!


Ukitaka maelekezo mengine ya ndani ndani, namna inavyofanya kazi wapi vipi, nk, unaeza kutazama hii video


May be ukitaka kuelewa zaidi kuhusu huo uchawi wa Piezo ambao Pressure sensor nyingi zinategemea, bonyeza HAPA kwenye hii link au picha hapa chine LINK


Sensor hiyo mara nyingi inaka namna hii

Jinsi yalivyoelezwa yote kwenye hizo video, sensor hii inaweza kuwa na waya tatu au waya nne.

Mara nyingi reference voltage inakuwaga 5V kutoka kwenye ECU!

Weka igntion-ON, chunguza umeme kwenye hizo waya!

 

CONTROL SYSTEMS (intro)

Siku hizi almost kila kitu kinaundwa kuwa na hii blaa bla ya CONTROL SYSTEMS, mfano, AC za ofisini, nyumbani mataa yanajiwasha yenyewe, gari za siku hizi kila kitu mafundi wanazungumza ‘kontulo’ yaani control (ECU) ama kompyuta ya gari, nk!

Hapa tunaelezana kwa ufupi, maana na jinsi, au namna huu uchawi wa CONTROL SYSTEM unakuwa!

Imagine huu mfumo wa hesabu

X + 5 = Y

(5 haibadiriki, lakini X au na Y inaeza kuwa chechote)!
X ikiwa 2, ina maana Y itakuwa 7
2 + 5 = 7
Ina maana ukitaka mfumo wako uwe tu wenye 7 kama matokeo, lazima X uingize iwe 2, au na vinginevyo! Ukitaka matokeo au Y iwe 9, hapo lazima X iongezeke kuwa 4!

Tayari, hapa 5 ni control!
Huo mfumo 5 (control) kudhibiti matokeo kwenye Y(output) kulingana X (input) itakachokuwa, ni CONTROL SYSTEM wa X + 5 = Y

CONTROL SYSTEM ni mfumo ambao matokeo yanategemea maingizo!Kwa mfano wetu pale juu,
Input  ni X, Control ni 5, alafu Output ni Y!

Alafu hizi CONTROL SYSTEMS zinaundwa kwa aina au namna mbili! Kuna zile ambao hamna aja ya kuthibitisha au ku comfirm matokeo, a.k.a OPEN LOOP CONTROL SYSTEMS, alafu na zile ambao lazima, au ata matokeo yanafanya uchawi ata kwenye mainginzo, ambao ni CLOSED LOOP CONTROL SYSTEM!

Naomba, ili kueleezana viruzi tofauti kati ya hizi aina, kutumisa mfano wa ile AC ya kudhibiti ujoto chumbani au ata ikiwa gari!

OPEN LOOP CONTROL SYSTEM

Imagine, hiyo siginal ya INPUT inatokea kwenye Temperature sensor inaochunguza ujoto chumbani au ata kwenye gari, mfumo ni kwamba hiyo Temperature sensor ikipeleka umbea kwamba kuna ujoto chumbani, hapo AC itaanza, yaani itawaka tu, hata kama hakuna mtu yeyote chumbani! Sasa ndo hizi OPEN LOOP CONTROL SYSTEM!

CLOSED LOOP CONTROL SYSTEM

Sasa hiyo siginal ya INPUT inatokea kwenye Temperature sensor imeruhusu AC kuanza, lakini AC ikiwaka lazima kuna ijulishe au ipeleke umbea kwamba nimewaka! Sasa huko sehemu ndo kuna blaa blla zingine kuchunguza kama kuna watu au la, ikiwa la AC itajizima yenyewe! Huo mzunguko ndo CLOSED LOOP CONTROL SYSTEM!

Kukitokea mfano tatizo, tuseme huku AC inawaka hata bila watu au vinginevyo, ukifanya diagnosis hizo blaa blaa za OPEN LOOP detected!


GROUND, NEUTRAL, EARTH, connections explained

Hata kama EARTH na GROUND ni kama kitu kimoja, lakini ni tofauti!
Kwa kingereza ya Merikani wanasema GROUND, alafu kwa Kingereza ya Ulaya(Europe) ni EARTH, so sometimes maana inakuwa confused!
So is why we tried to explain the difference in this video


ufafanuzi wa MANENO fulani ya kitaalam

Hapa tunajaribu kufafananua au kuelezeana maana ya maneno fulani ya kitaaalam👌, ambao tunatumia katika maisha yetu ya kila siku, bila kujua maana🤔!
So, HAPA UJANJA tu👨‍🎓