APP sensor (Accelerator Pedal Position Sensor)

Accelator Position Sensor, au ‘sensa’ ya kanyagio cha kuongeza kasi ya gari, namna jina ilivyo, inapeleka umbea kuhusu kiwango dereva amakanyaga ki kanyagio, kwenda kwenye kompyuta ya gari! Sasa, kulingana na habari hii, kompyuta itajua niaje kuhusu kiasi cha mafuta cha mafuta uachiliwa kuchomwa, obviously na kiasi gani cha hewa ile throttle iwachilie!
Sensoryenyewe ipo hapo, juu ya kanyagio!

Moduli ya kanyagio inaweza kuundwa kwa uchawi wa, potentiometer au wa Magnetic Hall Effect, kulingana, au namna hii video itakuonesha ndani zaidi! Namna yeyote, lakini Sensor hii inasajili fasta fasta harakati na msimamo wa kanyagio cha kuongeza kasi.


May be ukitaka ‘kulewa’ zaidi sana kuhusu huo uchawi wa Magnetic Hall Effect, bonyeza tu HAPA au kwenye hii picha chini!

Jinsi umeelewa, au kukumbuka, hii sensor inapeleka umbea kwenye kompyuta ya gari, alafu kompyuta inamuambia Throtle kiasi ya kufunguka, obviously na blaa bla zingine kwenye CAN, kiasi cha mafuta kinachohitajika, kulingana…
Na sababu kwanini zinakuanga sensor mbili ndani ya moja, au?

Sawa, jinsi tumejua kompyuta au ECU inatuma umeme 5V kuzungukia kwenye kila moja ya hizi sensor nani ya APP sensor, na juu ya huo uchawi w
a Hall Effect au Variable Resistance, kulingana kiasi ya mzunguko ata resistance itabadilika!
Sasa, wakati unapima, ukiona waya 6, lazima upate 5V mbili, ground au negative mbili, na siginal ….mbi?

 

MAP sensor

MAP sensor, au, Manifold Absolute Pressure Sensor, inapima kiasi au uzito wa mkusanyiko wa hewa uliopo kwenye ‘intake manifold’!
Mkusanyo wa hewa ukijumulisha na hewa inaotoka njia za mfumo zingine kama, EGR, TURBO, PCV, nk!Manifold ni hicho ki bla blaa kabla hewa kuingia cylinder au baada ya Throttle

Hii sensor inaeza kuwekwa popote, kulingana gari, ili mradi kuna njia yakufikia kupima hiyo hewa!


Ukitaka maelekezo mengine ya ndani ndani, namna inavyofanya kazi wapi vipi, nk, unaeza kutazama hii video


May be ukitaka kuelewa zaidi kuhusu huo uchawi wa Piezo ambao Pressure sensor nyingi zinategemea, bonyeza HAPA kwenye hii link au picha hapa chine LINK


Sensor hiyo mara nyingi inaka namna hii

Jinsi yalivyoelezwa yote kwenye hizo video, sensor hii inaweza kuwa na waya tatu au waya nne.

Mara nyingi reference voltage inakuwaga 5V kutoka kwenye ECU!

Weka igntion-ON, chunguza umeme kwenye hizo waya!

MASS AIRFLOW SENSOR

Jina kamili la hii Sensor ni, Mass Air Flow Sensor! Kwa wengi inajulikana zaidi kama MAF sensor, mara Air Mass, nk! Ingawa inaweza kuwa na majina mengi, inawajibika kwa kazi moja tu, kupima kiasi cha hewa, na ujoto wa hiyo hewa, inayoingia kwenye injini, na kupeleka taarifa hii kwenye kompyuta ya gari, yaani ECU au PCM au ‘kontulo boxi’!
Kompyuta au ECU kulingfana hii taarifa, ndo itajua kiasi gani cha mafuta kinachohitajika!

Hii sensor imewekwa kwenye bomba la uingizaji hewa, baada ya chujio au filter ya kusafisha hewa! Hapo chini kuna video inaonesha kila so tunafanya maandishi haya kuwa mafupi, chini kwenye hii page tunakupa muhtasari mafupi au summary, ikiwa ungependa maelezo zaidi, unaweza kutazama video! Kwenye video kuna blaa blaa ya aina za hii sensor!


HAPA NDO VIDEO UKITAKA KUTAZAMA ULEWE ZAIDI


Nadhani umehelewa kwanini zingine utakuta zina waya moja, mbili, zingine tatu, zingine nne, tano, sita, nk!
Zikwa waya tatu au nne inakuwa tu Air flow meter ya kupima tu uzito!


Ikiwa way moja au mbili inakuwa tu Intake Air Temperature ya kupima tu ujoto wa hewa inaoingia!
ECU inatuma 5V zizungunkie kwenye hii sensor, kulingana mbadiliko ya resistance, hapo ECU iatajua kama ni mazingira ya baridi au moto!


Na zikiwa tano au ata sita, kumanisha Airflow Meter pamoja na Intake Air Temperature, au Mass AirFlow SensorECU inatuma +5V na -5V zizungukie kwenye upande wa IAT katika hii sensor!
MAF power (+) inatokea battery moja kwa moja ikiwa switch ON! Ground ya MAF inakuwa ya kugawana!
MAF siginal ndo inaenda kwa ECU, Negative au Ground ya siginal inapatikana automatically, hahahahahhah…


Lakini, kwenye mfimo mingine, unaezakuta hakuna upande wa IAT sensor, inakuwa upande wa kupima uzito tu! Waya zote nne zinakuwa niaje kama hapa chini!


Au kugawana waya moja GROUND, lakini kila kitatoka kwenye ECU

Translate /Tafsir /Traduire