Accelator Position Sensor, au ‘sensa’ ya kanyagio cha kuongeza kasi ya gari, namna jina ilivyo, inapeleka umbea kuhusu kiwango dereva amakanyaga ki kanyagio, kwenda kwenye kompyuta ya gari! Sasa, kulingana na habari hii, kompyuta itajua niaje kuhusu kiasi cha mafuta cha mafuta uachiliwa kuchomwa, obviously na kiasi gani cha hewa ile throttle iwachilie!
Sensoryenyewe ipo hapo, juu ya kanyagio!
Moduli ya kanyagio inaweza kuundwa kwa uchawi wa, potentiometer au wa Magnetic Hall Effect, kulingana, au namna hii video itakuonesha ndani zaidi! Namna yeyote, lakini Sensor hii inasajili fasta fasta harakati na msimamo wa kanyagio cha kuongeza kasi.
May be ukitaka ‘kulewa’ zaidi sana kuhusu huo uchawi wa Magnetic Hall Effect, bonyeza tu HAPA au kwenye hii picha chini!
Jinsi umeelewa, au kukumbuka, hii sensor inapeleka umbea kwenye kompyuta ya gari, alafu kompyuta inamuambia Throtle kiasi ya kufunguka, obviously na blaa bla zingine kwenye CAN, kiasi cha mafuta kinachohitajika, kulingana… Na sababu kwanini zinakuanga sensor mbili ndani ya moja, au?
Sawa, jinsi tumejua kompyuta au ECU inatuma umeme 5V kuzungukia kwenye kila moja ya hizi sensor nani ya APP sensor, na juu ya huo uchawi w
a Hall Effect au Variable Resistance, kulingana kiasi ya mzunguko ata resistance itabadilika!
Sasa, wakati unapima, ukiona waya 6, lazima upate 5V mbili, ground au negative mbili, na siginal ….mbi?
MAP sensor, au, Manifold Absolute Pressure Sensor, inapima kiasi au uzito wa mkusanyiko wa hewa uliopo kwenye ‘intake manifold’!
Mkusanyo wa hewa ukijumulisha na hewa inaotoka njia za mfumo zingine kama, EGR, TURBO, PCV, nk!Manifold ni hicho ki bla blaa kabla hewa kuingia cylinder au baada ya Throttle
Hii sensor inaeza kuwekwa popote, kulingana gari, ili mradi kuna njia yakufikia kupima hiyo hewa!
Ukitaka maelekezo mengine ya ndani ndani, namna inavyofanya kazi wapi vipi, nk, unaeza kutazama hii video
May be ukitaka kuelewa zaidi kuhusu huo uchawi wa Piezo ambao Pressure sensor nyingi zinategemea, bonyeza HAPA kwenye hii link au picha hapa chine LINK
Sensor hiyo mara nyingi inaka namna hii
Jinsi yalivyoelezwa yote kwenye hizo video, sensor hii inaweza kuwa na waya tatu au waya nne.
Mara nyingi reference voltage inakuwaga 5V kutoka kwenye ECU!
ย As you know, diagnostics, or fault finding, is a fundamental part of an automotive technician’s work, and as automotive systems become increasingly complex there is a greater need for better diagnostic skills.
This very Advanced Automotive Fault Diagnosis is a better book to treat automotive diagnostics as a science rather than a check-list procedure.
As breifly shown, each chapter includes basic principles and examples of a vehicle system followed by the appropriate diagnostic techniques, complete with useful diagrams, flow charts, case studies and self-assessment questions.
The book will help new students develop diagnostic skills and help experienced technicians improve even further. This new edition is fully updated to the latest technological developments.
Along with more new real-life case studies, this edition of Advanced Automotive Fault Diagnosis includes new content on diagnostic tools and equipment: VCDS, decade boxes, scanners, pass through, sensor simulators, break out boxes, multimeter updates for HV use, and more .
It explains the fundamentals of vehicle systems and components, and it examines diagnostic principles and the latest techniques employed in effective vehicle maintenance and repair.
Diagnostics, or faultfinding, is an essential part of an automotive technician’s work, and as automotive systems become increasingly complex there is a greater need for better diagnostic skills.
This list is very incomplete, tunaendelea kuweka๐ค! So, ukikosa uliotaka, shuka chini ya hii page utujulishe tukutumie fasta fasta, au zungumza/chat withย SUZANย if She is online!ย HAPA UJANJA tu๐!
This is COMPLETE official OEM full workshop service repair manual containing easy-to-read text sections with top quality diagrams and instructions includes: Detailed sub-steps expand on repair procedure information,
Notes cautions and warnings throughout each chapter pinpoint critical information,
Numbered instructions guide you through every repair procedure step by step,
Bold figure number help you quickly match illustrations with instructions,
Detailed illustrations, drawings and photos guide you through every procedure,
Enlarged inset helps you identify and examine parts in detail,
Numbered table of contents is easy to use so that you can find the information you need it fastly,
Troubleshooting and electrical service procedures are combined with detailed wiring diagrams for ease of use and to makes it easy to repair problems with your carโs electrical system!
You may watch this video showing you the contents, after go below the video to download!
Unaeza kuwa una hiyo diagnosis mashine, but kunachangamoto unapata๐ค! May be matumizi ya namna kufanya utundu fulani wa kitaalamu, auย inaeza kuwa mashine ina tatizo imekushinda kurekebisha, au, meeeeeen, could be any problem๐คทโโ๏ธ! So tunaweka hapa kila taka taka tunakutanayo zinasumbua watumizi mbali mbali๐!
Tunawekanga namna ya kupata software za mashine, au ukitaka ku update au downdate au kuharibu mashine tunakuonesha unafanyaje๐คทโโ๏ธ! Ukitaka password za ku login mtandaoni (cloud diagnosis) zote tunawezasaidiana๐!
The purpose of this section is to help you understand the general diagnostic process that you will follow regardless of the type of customer concern you are troubleshooting…..and also to know about the features of diagnostic tools that will help you with greater accuracy
and speed…..not forgeting the lay out the troubleshooting steps and resources you will need to follow when diagnosing customer concerns.
Hybrid Vehicle Powertrain Systems combine conventional powertrain components, an internal combustion engine and transmission, with new electric components, electric motor, power electronics and high voltage energy storage, such as a battery.ย So this from TOYOTA engineer is to help you know how to perform the necessary maintenance, service, and repair procedures on hybrid cars!
This manual is about that direct petrol injection and ignition system (4cyl. 2.0 ltr. 4-valve turbo) and it is, this is designed to help you perform necessary diagnostics, maintenance, service, and repair procedures on any applicable AUDI engines! Infact better download and even print out this manual, necessarily๐คทโโ๏ธ
Hiki kitabu kinajaribu kufafanunlia maana ya OBD fault code, wapi tatizo lilipo kwenye gari, pamoja na umbea wa ziada wenye namna tofauti tofauti chakufanya ili kutatua hilo tatizo! So try go through it, uone kama kinaeza kuwa kitabu mhimu kwako! Kama kuna maneno ya kingereza huelewi, tumisa ile app ya kutafsiri maana!
Haka ka software kako na zile basics za OBD blaa blaa, ufanyaji kazi wa ma sensors, actuators, codes, nk! Picha/maneno mengi ya kitoto lakini huwezijua may be kanaweza kusaidia๐คทโโ๏ธ! Alafu kanafunguka tu kwa computer sio simu๐!
ENGINE SPEED inamanisha mwendo engine inazunguka (a.k.a RPM) alafu VEHICLE SPEED ni mwendo wa gari zima au tuseme muzunguko wa tayari although sio! Hizi sigina zinakuwa programmed tofauti tofauti as shown in this nonsense video!
Gari za siku hizi ni kama mwili wa mwanadamu๐ค! Sasa, CAN BUS ni kama ni mfumo wa neva, yaani nervous system, unaowezesha mawasiliano wa kila mfumo wa mwili!
Ndiyo, hizo ECU zione kama vipande vya mwili vilioonganiswa na huu mfumo wa CAN BUS!
CAN BUS (CAN = Controller Area Network) alafu BUS ni kama basi la abiria munaingia wengi lakini kila atashuka sehemu tofauti, kulingana!
So, CAN ni muungano wa ma kompyuta ziliopo kwenye gari kwamba zinawasiliana, kupeana msaada!
Mfano, kompyuta au ECU ya SUSPENSION ikihitaji umbea kuhusu speed, mwendo wa gari, itapata umbea huu kwa CAN juu computer ya ABS yenye speed sensor zinazochunguza mwendo wa gari itaweka signal hii kwenye CAN kuliko kwamba speed sensor zitafungwa kwa kila computer ya gari itahitaji mwendo wa gari๐!
You may watch๐๐this video for deeper explanation!
Tunapata mada yoyote kulingana, kisha tunajadili (discuss) kikamilifu kwa njia ya kawaida mtu yeyote anaweza kuelewa …na mazoezi pia! Hii sio jinsi shule za kawaida zinafundisha, but how the real world is๐ค so You use whatever You learn to solve real problems around You!
COMPUTER ni kifaa cha elektroniki keyenye uwezo wa kupokea ujumbe na kufanya kazi kwa huo ujumbe kulingana maagizo๐ค, kiisha kutoa/kuonesha matokeo!
Huu ni umbea kwanzia kama computer mbili kwenye room moja kuwezaje kuwasiliana, then may be computer kwenye room tofauti au nyumba tofauto au mji tofauti mpaka mpaka computer zikiwa bara (continet) mbali mbali zinawezaje kuwasiliana! Alafu tukisema computer, ione kama simu au TV au chechote kinachokuwezesha kuwasiliana!
MAC address ni kama kitambulisho cha kifa (a.k.a network interface controller ) kinachowezesa kitu chechote kuweza kuungana kwenye (mtandao) network ili kuwasiliana vitu vingine! Hicho ‘kitu chechote’ kinaweza kuwa simu, laptop, printer, gari, nk as long it can connect to any network!
Nguvu za magineti๐ zikija karibu kwa wire au kifaa chechote kinachopitisha umeme na kwamba kuna umeme unaopita๐คkwa hiki kifaa, kuna uchawi funi utakaotokea kusababisha/kuzalisha umeme namna tulivyolekezana kwa hii video๐! Kwasabu kwa maneno sijui niekwelekezeaje na maneno gani๐ aiiise!
Electronic Stability Program (ESP) ama Electronic Stability Control (ESC), au tena Dynamic Stability Control (DSC), ni uchawi wa ku improve a computerised vehicle’s stability by detecting and reducing loss of traction (skidding). ESP baada ya ku detect any loss of steering control, kuna namna it applies the brakes kuifanya gari irudi where the driver intends to go bila kupagawa namna tulijaribu kuelezea!
Nguvu za ule moshi unaotoka kwa engine unatumika kuzungusha aina ya kama pampu fulani hivi, na wakati wakuzunguka hii pump inanyonya au kuvuta hewa kutoka nje ya gari ili kuongeza kiasi cha hewa engine inahitaji kufanya kazi vizuri namna tulijaribu kueleza humu! Na pia kuna hizo pressure sensors, temperature sensor, nk๐คท๐ผโโ๏ธ !
AIRBAG system iko na sensa ya kuchunguza kutikisa, ina maaana gari ikitikisa gafla kupiita kiasi, hii sensa itapeleka umbea kwa ECU (control boxi)!
Sasa, ECU ikipata itapeleka moto (power) kwa defletor na kulipuwa AIRBAGย namna tulijaribu kuoneshana hapa๐pamojaย na chakufanya iliย kutoa/kuziima hiyo taa ya AIRBAG๐จโ๐ง
Watu wengi wamebadilisha mafuta (OIL) ya gari lao wenyewe au wamepeleka gari kwa garage kwa wataalamu! Sasa, kipengele muhimu kuhusu blaa blaa ya mafuta (OIL) ni kuchagua aina ya OIL sahihi pamoja na right quantity๐ค! I swear, unahitaji kuzingatia nambari zilizo kwenye lebo ya mafuta (OIL) ya gari. Unaweza kuona kitu kama “10W30” au “5W20” na ukashangaa wanamaanisha nini hiki๐๐๐คฃ๐๐๐ .
Sii unajua kuna maelekezo jinsi ya kufungua, kufunga, kurekebisha, ku fanya hiki na kile…pamoja na michoro ya wiring, picha zote๐! Iliaandaliwa na wataalamu wenyewe๐, so…..?
Hebu tazama hii video uone niaje๐, kiisha shuka chini uweze kui download!
Mercedes Benz wanatoa umbea, ujuzi, ujanja wooooote, kuhusu wakati gani, kwa nini, utumise nini, yaaani, jinsi ya kugundua, kutatuta magari yao pamoja na michoro ya waya, picha ya kia kitu!
So, tumekuwekea yote hapa, kwamba ata hii APP unaeza kuitumia kwenye ๐ฒsimu yako ya popte ulipo unapozunguka!
Like, wakati unapima BENZ kuna vi code code wanaotumia vya kumanisha kitu gani kwenye gari๐คท๐ผโโ๏ธ!
Mfano, kumanisha fuel pump wanweza kuweka code FP17/QU so kama hujui FP17/QU inamanisha kitu gani na kiko wapi๐, unakwamma tu!
HAPA UJANJA tu! Ata kwa๐ฒsimu unatumia๐ Tazama hii video uone namna kwenye simu๐ฒ
Ukitaka kwenye simu๐ฒ ama tuseme iwe mobile kwamba popote ulipo ๐ฒ!
๐๐๐
Huu uchawi wa PIZOELECTRIC EFFECT ni kwamba, ukigonga au kukandamiza kitu kiliotengenezwa kwa ile kemikali ya crystal blaa blaa๐๐คฃ๐, hicho kitu kinaweza kuzaa umeme. TENA ukipitisha umeme katika hicho kitu, kitatemeka (to vibrate/shake or move)! So ni vice versa namna tulijaribu kuoneshana kwenye hii video๐คท๐ผโโ๏ธ
Kwa kutaka kuongeza nguvu za magari, bila kutumisa mafuta mengi, pamoja na bila kuharibu mazingira๐ค, wataalamu waligundua namna ya kuchunguza mafuta na hewa inaoingia kwenye engine…pamoja na kuchunguza huo moshi unaotoka kwa engine๐ ili husiharibu mazingira nje ya gari. So waliweka sensor za kuchunguza na kupeleka umbea kwenye ECU/control box (computer), alafu ndo computer iwaambie actuators kazi ya kufanya, kulingana๐คท๐ผโโ๏ธ! Sasa, kwasababu engine ya gari inategemea mafuta na hewa ili kuweza kufanya kazi, ndo maana njia za mafuta na hewa pamoja na hewa chafu (moshi) waliweka hizo sensor na actutors! So we shall look at all the sensors on in each systems as ellaborated in this video
AIRFLOW METER SENSOR
Either hii sensor inapima tu ujoto, AU inapima ujoto pamoja na uzito wa hewa inaoingia ndo hapo inaitwa Mass Airflow meter sensor!
Ikiwa inapima tu ujoto inakuwa na wire 2 tu
Iiwa inapima ujoto na uzito wa hewa, inaweza kuwa na๐ค,
> 5 wires (2 yakupima joto, 3 za kupima uzito)
>4 wires (ground au negative wire ya upande wa kupima joto iko pamoja na ya upande wa kupima uzito)
>3 wires hakuna upande wakupima ujoto, inapima tu uzito wa hewa!
Hii video tuloneshana namna sensor inafanya kazi, pamoja na kupimwa ikiwa natatizo๐ฉ๐ผโ๐ง
MANIFOLD ABSOLUTE PRESSURE SENSOR (MAP)
Hewa ikifika kwenye inlet manifold itakutana hewa ingine inaotokea njia zingine kama Turbo, EGR, EVAP system, nk! Ina maana lazima au bora kuwepo namna ya kupima jumla ya hewa iliopo kwenye manifold kabla kuingia kwenye engine๐ค hapo ECU ama control ijue kiasi cha mafuta itafanya injector zitoe๐! So, hii MANIFOLD PRESSURE SENSOR ndo inapima jumla ya hewa iliopo kwenye inlet manifold! Hii sensor mara nyigi ni 3 wires๐ค, moja ni 12V au 5V, ingine ni Negative/ground, Ingine ni ya SignalHii sensor ilitengenezwa kwa uchwa waPIEZOELECTRIC EFFECT, ukibonyeza hapatulijaribu kuonesha maana ya huu uchawi
Otherwise nama hii sensor inafanya kazi na kupimwa ili kujua kama ina tatizo, tulijaribu kuineshana katika hii video
ACCELERATOR PEDAL POSITION SENSOR
Sii ujajua hizi gari za kisasa kile ki pedal ni cha umemeโก tofauti kwa zile gari za zamani kulikuanga ka metal fulani๐Sasa hii sensor ina sensor mbili kwa moja, because the other ni ya emegency kama upande moja ukiharibika, namna ya ufanyaji kazi na kupimwa in this video๐
Baada ya kuganyaga kwenye accelerator pedal umbea unapelekwa kwa ECU (control box) ili ijue namna ya kunfungua hiki ki blaa blaa THROTTLE cha kuruhusu hewa ingie kwenye Engine! Hii ELECTRONIC THROTTLE CONTROL iko na kile kiko ka ulimi ya mtu hiivi kufungua na kufunga๐คท๐ผโโ๏ธ! Kuna mota (motor) ya kutembeza hiki ki ulimi!ย Na kuna sensor ya kuchunguza hiki ki ulimi kimefunguka kiasi gani๐ค!
Namna ya kupima AND ufanji kazi tazama hii video๐
Bila kufunga mfuniko wa kwenye tenki la mafuta, inasababisha upepo wa nje kuingia au ata mafuta kupotea kwa nja ya upepo (Evaporation)๐! Sasa, ili kuhakisha unafunga mfuniko wa tenki, kuna sensa iliwekwa ili kwamba usipofunga, kuna taa itaonesha kwenye instrument cluster au ata taa ya check-engine yenyewe…au kuna uchawi ECU inafanya kwenye gari ili isitembee vizuri mpaka ufunge huu mfuniko๐!
Jinsi unavyojua๐, ukiweka kitu chochote kilivyo kama maji (liquid substance) kwenye kama dumu hivi, ukichezesha (shake) hiyo dumu, kuna pressure inatokea! Sasa, ata maafuta kwenye tenki la gari, kila gari ikitembea obviously inacheza so yale mafuta kuna uchawi unatokea kuyafanya kubadilika kuwa ya upepo na kuongeza pressure kwenye tenki, ndo maana kuna FUEL TANK PRESSURE SENSOR yakuchunguza kiasi cha pressure kwenye tenki๐!
Hii sensor ilitengenezwa kwa uchwa waPIEZOELECTRIC EFFECT, ukibonyeza hapatulijaribu kuonesha maana ya huu uchawi, so na maana ina 3wires๐คท๐ผโโ๏ธ
Wakati gari inatembea, inachezesa tenki na kufanya yale mafuta (kama maji) kubadilika au ku evaporate kuwa upepo๐ค! Sasa, hii EVAP SYSTEM inaosaidia kufanya uchawi ili yale mafuta ya upepo yasichanganyike au yasiende kwenye njia ya mafuta ya maji! Hii EVAP SYSTEM iko na njia mbadala yakupitisha upepo kwenda kwenye manifold au nje ya gari kulingana๐จ!
Kuna ile meter ya kuchunguza kiasi cha mafuta kwenye tenki (tank), kuna pump, kuna ka sieve ka kusfisha hayo mafuta, na๐ค….jinsi tuanelekezana kwa hii video๐!
FUEL PRESSURE REGULATOR
Zamani, kwenye mfumo wa mafuta ya gari kulikuwanga pipe ya kurudisha mafuta kwenye tenki yakibaki, sasa kwa hizi gari mpya kuna sensor yakuchunguza kiasi cha mafuta yanaohitajika NA ndo hayo mafuta yatakaporuhusiwa kutoka! Ndo sababu ingine kwanini unaona ka pipe moja kwenye tenki! Sasa, tulijaribu kumbushana uchawi kwenye FUEL PRESSURE REGULATOR๐จโ๐ง
Ukitoa mugu kwenye accelerator pedal (ile yakuongeza nguvu ya gari) ata ule mfuniko wa kuruhusu hewa ingie kwa engine unaziba๐ค ina maana engine ikikosa hewa itazimika๐คท๐ผโโ๏ธ! Sasa uchawi wa IAC valve ni kufungua ka njia fulani ile hewa ipite kufika kwa engine ata ukitoa muugu๐ au tuseme ukitoka kwa gari inaendelea kuaka!
Assuming kwamba unajua crankshaft au camshaft ni nini, sasa ili kuweza kujua muda gani wakati cylinder fulani inafanya kitu gani na inahitaji nini, hizi CAMSHAFT na CRANKSHAFT POSITION SENSOR kuna uchawi unaziwezesha kujua ipi niaje, na kupleka huu umbea kwenye computer ya gari namna tulijaribu kumbushana au kuoneshana๐ป
Jinsi unavyojua, kifaa chenye uwezo kutembeza umeme kinabadilika kulingana ujoto au ubaridi๐ค! So computer ya gari inatuma umeme kuzunguka kwenye hii ENGINE COOLANT TEMPERATURE SENSOR , kuligana ujoto/ubaridi umeme (volts) zitazorudi kwa computer, either itapungua au kubaki niaje namana tulioneshana๐จโ๐ง
Hii KNOCK SENSOR ione kama microphone, inachukua au kusikilizia sauti ya engine na kupelekea ECU (control box) umbea! Sasa kuna sauti ya kawaida ya engine ambao ECU imezoea, so like mafuta + hewa yakichomwa kwa muda au mahali ambao sio sahihi ya kwamba sauti ya engine itabadilika, hapo ECU ikipata sauti tofauti ya engine kupitia hii KNOCK SENSOR itajua kuna uchawi wa engine knock (a.k.a detonation) umetokea!
Obviously unafahamu kwamba baada ya engine kuchoma mafuta + hewa kuna moshi unaotokea๐ค, sii unajua au unaona huo moshini chafu, lakini huu moshi unafanywa kuzunguka kurudi au kuungana na ile hewa safi inaotokea nje gari! Sasa, huu moshi kufanywa kuzunguka na kurudi kwenye engine kuna uchawi mwingi unatokea, kama kushusha temperature ya engine, kupunguza moshi unaotoka nje ya gari ili usiharibu mazingira, na blaa blaa blaa zingine! Sasa hii EGR system unakuta kuna sensor & actuator nyigi ambao unapswa kujua au kumbuka๐จโ๐ง!
Jinsi unafahamu, engine inahitaji mafuta & hewa ili vichanganyike vichomwe ndo engine ipata nguvu๐, ndiyo lakini kuna namna hewa & mafuta yanapaswa kuchanganyikwa (a.k.a stoichiometric ratio) as in kukiwepo mafuta lita 1 lazima hewa iwe kama lita 15๐คท๐ผโโ๏ธ! Sasa, kukitokea na pamoja kuzuia uchawi kama mafuta yanakuja mengi au madogo, kuna hizi OXYGEN SENSOR ambao zinachunguza moshi unaotokea baada ya mafuta + hewa kuchomwa, so huu umbea unahusiana kuhusu hizo OXYGEN SENSOR, ziko wapi, zinafanyaje kazi, kupima nini, na blaa blaa zingine๐!
Sii unajua ufanyaji kazi wa engine, piston inanyonya hewa+mafuta alafu inagandamiza (compress) then blaa blaa kuchoma๐ง, sasa kwenye kugandamiza (compress) kuna hewa + mafuta ina bypass kati ya piston na cylinder wall kujikuta kwenye sump (dumu ya oil chini ya engine)! Sasa kutoa hii hewa kuna ka pipe kanawekwa ili kunyonya huu upepepo as we tried show in here๐ฌ
Kwenye AUTO TRANSMISSION, uchawi zaidi zaidi ni wa valve ambao valve zinategemea solenoid, zingine ni pressure sensor na temperature sensor! SO, kama ulihelewa vizuri kuhusu blaa blaa za hizi sensor kwenye system zingine, then ili muradi picha inakuonesha hii sensor iko wapi, then troubleshooting AUTOMATIC TRANSMISSION troubles ni kama kunywa maji๐ป!
Uchawi kuweza blaa blaa ya ma sensor, control boxi, sijui actuators ni kujua mfano ni sensor gani, iko wapi, inafanya kazi gani, inafanyaje hiyo kazi as in iliundwaje (how it is made), nk! So ukipata umbea huu wote ndo utajua inahitaji kupeleka au kutoa umeme gani kutoka wapi au blaa blaa as we explained in here๐จ๐ผโ๐ !
Jinsi hii video inakuonesha, hiki kitabu kina namna ya ku program funguo za gari, mashine gani yakutumia, vifa gani vya kufungua/kufunga kwenye gari, nk! Yaani unapata almost kila umbea mhimu๐!
Technologia inabadilika kila sekunde, so ukiona mashine fulani ndo ilitumika, usikulupuke kununua hiyo mashine unaezakuta kuna mashine ingine mpya/bora! Hiki kitabu kikusadie tu kutoa mwanga kwa macho yako, nenda ufanye research nyingi zingine bora๐๐ผ!
Kwanza moja kwa moja, ukumbuke how immobilizer systems work, what components involved, why and how to supercalifragilisticexpialidocious if lost or spare keys๐คทโโ๏ธ
Kwanzia hizo TRANSPONDER KEYS funguo za chuma za kawaida, mpaka hizo SMART KEY, tunaanza na mifumo, jinsi zinafanya kazi, ili uweze kuelewa kwanini, mashine fulani ndo zinazo kamilisha kazi fulani!
TRANSPONDER KEYS
Kwa kutaka kuzuia wizi, walifanya uchawi kwenye gari kwamba isipo kuwa funguo maalum ya hiyo gari maalum, hiyo gari haiwezi kuendeshwa. Kwenye funguo waliweka kadude fulani kanaitwa Transponder Sasa haka kadude namna tulivyoneshana kwa video, kuna neno siri ama PIN a.k.a password ambao lazima ifanane na ilyo kwenye gari. Isipo fanana gari haitawaka!
So, kwa hii video tulijaribu kuoneshana namna hiizi blaa blaa zote zinafanya kazi
Ina maana hiyo funguo maalum ya kuendesha gari maalum ikipotea lazima ufanye uchawi wa ziada kuirudisha namna tuliojaribu kumbushana katika hii video!
ONYO๐จ: Mara kwa mara kuna ujanja unaotokea wa nmna ya kufanya key programming, so hii ni just basics of what could be done in case๐คทโโ๏ธ!
TRANSPONDER DETAILS
Na hata kama hizo transponder zinafanana kwa muonekano, lakini ziko tofauti kaaabisa! Yaani ziko na namba mf., ID46, 4C, TPX7, nk kulingana aina ya gari! Ina maana ukileta tranponder ya Toyota Corona kuiweka kwa system ya Toyota Carina, hazitafanya๐คท๐ผโโ๏ธ namna tulioneshana kwenye hii video
Sasa kuna system zenye funguo za transpoder kama tumeone, na kuna smart key systems
SMART KEY SYSTEMS
Sasa, hizo smart zinabaki mfukoni kwamba unaeza kufungua mlango na kuendesha gari bila kuigusa hiyo funguo!
KEYLESS ama SAMRT KEY SYSTEM ina upande miwili, upande wa kuasha gari KEYLESS IGINITON SYSTEM, na upande mwingine wa tuseme kifahari hiiivi, KEYLESS ENTRY SYSTEM ile yakufungua mlango, booti, kutembeza viti, nk!
So namna hii video inakuonesha tutangaliza hizo part tofauti tofauti
KEYLESS IGINTION SYSTEM
Sasa tukianza na KEYLESS IGINTION SYSTEM tutaona namna SMART ECU ikishirikiana na ID CODE BOX, BODY ECU, ENGINE ECU, nk, kama TRANSMISION ECU, STEERING LOCK ECU, nk, ili kuwezesha engine kuaka kwa kutambua kama ndo funguo sahihi ilioko mfukoni ya huyo mtu anaejaribu kuendesha hiyo gari! Hii video ni ndeeefu pamoja na maneno mengi ya kurudia rudia ili uweze kuipata vizuri!
KEYLESS ENTRY SYSTEM
Sasa hapa tunajaribu kuoneshana KEYLESS ENTRY SYSTEM, utaona kwamba hapa ni SMART ECU na BODY ECU na componet zingine zinazohusiana…pamoja na uchawi gani unaweza kufanya kukitokea blaa blaa yeyote kwenye hii system!
Unajua kuna mashine nyigi na ni rahisi kutengeneza au kuongeza funguo ya smart. LAKINI ukikosea kidogo tu, ni hatari na kwamba system nzima utakuwa umehiharibu๐คทโโ๏ธ!
So be careful when diagnosising for problems or when using diagnosis machine as we tried ellaborate in this video
IMMO OFF & IMMOBILIZER DECODING
Kufanya IMMO OFF ni ule uchawi kufanya gari iwake na funguo yeyote kama kawaida au kama mifumo ya zamani.ย IMMOBILIZER DECODING๐, ni kama ufunguo umepotea, unafuta kumbu kumbu ya ufunguo, kuirudisha kuwa bikira (virgin) kama mwanamke akiwa ajaolewa, namna gari inavyokuwa kiwandani!
Namna tulioneshana kwenye hii video, kufanya IMMO OFF either unaweka emulator au ku edit data za IC ama chip ya funguo!
ONYO ๐
kama unajelewa niaje, mambo ya EEPROM data blaa blaa, tumekuwekea hapa data za IMMO OFF na DUMPS (virgin Data), otherwise endelea kujifunza niaje!ย
Na, sometimes, ukiwa na secret codes fulani, ziwe SMART KEYS au TRANSPONDER KEYS, kwa kutumia ata diagnosis machine ya kawaida, unaweza kufanya ujanja fulani!ย So, tumekuwekea program kuwezesha kupata hizo secret codes fulani!
Tena tulijua kwamba funguo ikipotea unaweza kupata code/passsword kutoka hiyo EEPROM ili ukatumbukize kwenye funguo ingine ndo gari iwake, au pia kama control boxi imekufa unatoa haka EEPROM ukaweke kwa hiyo control boxi ingine๐!
Sasa uchawi ni kusipojua EEPROM ya funguo iko wapi na ni gani katika hizo nyingi zilizopo kwenye circuit board, maana iwe control boxi au immo box kuna EEPROM nyingi nyingi.
So hii App๐ฒ ya kwenye simu au na kompyuta๐ป, inakusadia kujua EEPROM ipi au Transpoder ipi inaendana hiyo gari๐ค!
Sasa tayari umejua ni EEPROM gani ya funguo๐, je unajua nini chakufanya uweze kuisoma, kubadili ili ufanye IMMO OFF au DECODE ili kupata code/password ya funguo kutoka hiyo EEPROM?So ukibonyeza HAPA utona tulikumbushana au kuoneshana kuhusu data inakuanga humu, inakaje, inasomwa au kubadilishwa namna gani๐คท๐ผโโ๏ธ hizo blaa blaa binary, HEX, address, nk, mara Flash Memory, EEPROM memory, nk!
Hiki kitabu kina namna ya ku program funguo za gari, mashine gani yakutumia, vifa gani vya kufungua/kufunga kwenye gari, nk!
Yaani unapata almost kila umbea mhimu๐! Ni PDF๐ฒ popote๐ป kinafunguka!
Tuseme umepata idea ya namna funguo zinafanya๐!
Na funguo ikipotea umejua kwamba unaweza kutumia data ya EEPROM kuweza kutenegeza ufunguo mwingine AU ukafanya IMMO OFF ukatoa tu immo system ili gari ikubali funguo yeyote.
Sasa changamoto ni kujua uchawi gani wa kufanya immo off au ku program funguo ingine kwa kutumia data ya EEPROM ndo maana ukitaka niaje๐ข!
Tumekusanya kila aina ya programu, yaani software kufanya ujanja wowote kwenye kila gari๐ค, bonyeza tu HAPA HAPA HAPA๐คทโโ๏ธ!
Huu ni mifano namna hizi softyware ziliopo! Ni nyiiingi๐!
Zamani, kwenye mfumo wa mafuta ya gari kulikuwanga pipe ya kurudisha mafuta kwenye tenki yakibaki, sasa kwa hizi gari mpya kuna sensor yakuchunguza kiasi cha mafuta yanaohitajika NA ndo hayo mafuta yatakaporuhusiwa kutoka! Ndo sababu ingine kwanini unaona ka pipe moja kwenye tenki! Sasa, tulijaribu kumbushana uchawi kwenye FUEL PRESSURE REGULATOR๐จโ๐ง
#FUELPRESSUREREGULATOR #AUTOMOTIVEFUELSYSTEM #5021tips