AUTOMOTIVE ELECTRONICS (sensors, actuators, ECU,etc)

Kwa kutaka kuongeza nguvu za magari, bila kutumisa mafuta mengi, pamoja na bila kuharibu mazingira🤔, wataalamu waligundua namna ya kuchunguza mafuta na hewa inaoingia kwenye engine…pamoja na kuchunguza huo moshi unaotoka kwa engine🙄 ili husiharibu mazingira nje ya gari. So waliweka sensor za kuchunguza na kupeleka umbea kwenye ECU/control box (computer), alafu ndo computer iwaambie actuators kazi ya kufanya, kulingana🤷🏼‍♂️!
Sasa, kwasababu engine ya gari inategemea mafuta na hewa ili kuweza kufanya kazi, ndo maana njia za mafuta na hewa pamoja na hewa chafu (moshi) waliweka hizo sensor na actutors! So we shall look at all the sensors on in each systems as ellaborated in this video


AIRFLOW METER SENSOR

Either hii sensor inapima tu ujoto, AU inapima ujoto pamoja na uzito wa hewa inaoingia ndo hapo inaitwa Mass Airflow meter sensor!

Ikiwa inapima tu ujoto inakuwa na wire 2 tu

Iiwa inapima ujoto na uzito wa hewa, inaweza kuwa na🤔,
> 5 wires (2 yakupima joto, 3 za kupima uzito)
>4 wires (ground au negative wire ya upande wa kupima joto iko pamoja na ya upande wa kupima uzito)
>3 wires hakuna upande wakupima ujoto, inapima tu uzito wa hewa!

Hii video tuloneshana namna sensor inafanya kazi, pamoja na kupimwa ikiwa natatizo👩🏼‍🔧


MANIFOLD ABSOLUTE PRESSURE SENSOR (MAP)

Hewa ikifika kwenye inlet manifold itakutana hewa ingine inaotokea njia zingine kama Turbo, EGR, EVAP system, nk! Ina maana lazima au bora kuwepo namna ya kupima jumla ya hewa iliopo kwenye manifold kabla kuingia kwenye engine🤔 hapo ECU ama control ijue kiasi cha mafuta itafanya injector zitoe😎! So, hii MANIFOLD PRESSURE SENSOR ndo inapima jumla ya hewa iliopo kwenye inlet manifold!
Hii sensor mara nyigi ni 3 wires🤔,
moja ni 12V au 5V, ingine ni Negative/ground, Ingine ni ya SignalHii sensor ilitengenezwa kwa uchwa wa PIEZOELECTRIC EFFECT, ukibonyeza hapa tulijaribu kuonesha maana ya huu uchawi

Otherwise nama hii sensor inafanya kazi na kupimwa ili kujua kama ina tatizo, tulijaribu kuineshana katika hii video


ACCELERATOR PEDAL POSITION SENSOR

Sii ujajua hizi gari za kisasa kile ki pedal ni cha umeme⚡ tofauti kwa zile gari za zamani kulikuanga ka metal fulani🙄Sasa hii sensor ina sensor mbili kwa moja, because the other ni ya emegency kama upande moja ukiharibika, namna ya ufanyaji kazi na kupimwa in this video👇

#ACCELERATORPEDALSENSOR  #DRIVEbyWIRE  #5021tips


ELECTRONIC THROTTLE CONTROL

Baada ya kuganyaga kwenye accelerator pedal umbea unapelekwa kwa ECU (control box) ili ijue namna ya kunfungua hiki ki blaa blaa THROTTLE cha kuruhusu hewa ingie kwenye Engine! Hii ELECTRONIC THROTTLE CONTROL iko na kile kiko ka ulimi ya mtu hiivi kufungua na kufunga🤷🏼‍♂️! Kuna mota (motor) ya kutembeza hiki ki ulimi!  Na kuna sensor ya kuchunguza hiki ki ulimi kimefunguka kiasi gani🤔!
Namna ya kupima AND ufanji kazi tazama hii video😎

#THROTTLEbody #ENGINEsensors #5021tips


FUEL TANK-COVER SENSOR

Bila kufunga mfuniko wa kwenye tenki la mafuta, inasababisha upepo wa nje kuingia au ata mafuta kupotea kwa nja ya upepo (Evaporation)🙄! Sasa, ili kuhakisha unafunga mfuniko wa tenki, kuna sensa iliwekwa ili kwamba usipofunga, kuna taa itaonesha kwenye instrument cluster au ata taa ya check-engine yenyewe…au kuna uchawi ECU inafanya kwenye gari ili isitembee vizuri mpaka ufunge huu mfuniko😎!

#fueltankcover #automotivesensors #5021tips


FUEL TANK PRESSURE SENSOR

Jinsi unavyojua🙄, ukiweka kitu chochote kilivyo kama maji (liquid substance) kwenye kama dumu hivi, ukichezesha (shake) hiyo dumu, kuna pressure inatokea! Sasa, ata maafuta kwenye tenki la gari, kila gari ikitembea obviously inacheza so yale mafuta kuna uchawi unatokea kuyafanya kubadilika kuwa ya upepo na kuongeza pressure kwenye tenki, ndo maana kuna FUEL TANK PRESSURE SENSOR yakuchunguza kiasi cha pressure kwenye tenki😎!

Hii sensor ilitengenezwa kwa uchwa wa PIEZOELECTRIC EFFECT, ukibonyeza hapa tulijaribu kuonesha maana ya huu uchawi, so na maana ina 3wires🤷🏼‍♂️

Wakati gari inatembea, inachezesa tenki na kufanya yale mafuta (kama maji) kubadilika au ku evaporate kuwa upepo🤔! Sasa, hii EVAP SYSTEM inaosaidia kufanya uchawi ili yale mafuta ya upepo yasichanganyike au yasiende kwenye njia ya mafuta ya maji! Hii EVAP SYSTEM iko na njia mbadala yakupitisha upepo kwenda kwenye manifold au nje ya gari kulingana😨!

Kuna ile meter ya kuchunguza kiasi cha mafuta kwenye tenki (tank), kuna pump, kuna ka sieve ka kusfisha hayo mafuta, na🤔….jinsi tuanelekezana kwa hii video👇!


FUEL PRESSURE REGULATOR


 IDLE AIR CONTROL SYSTEM

Ukitoa mugu kwenye accelerator pedal (ile yakuongeza nguvu ya gari) ata ule mfuniko wa kuruhusu hewa ingie kwa engine unaziba🤐 ina maana engine ikikosa hewa itazimika🤷🏼‍♂️! Sasa uchawi wa IAC valve ni kufungua ka njia fulani ile hewa ipite kufika kwa engine ata ukitoa muugu👌 au tuseme ukitoka kwa gari inaendelea kuaka!

#IACvalve #ENGINEsensors #5021tips


CRANKSHAFT  & CAMSHAFT POSITION SENSORS

Assuming kwamba unajua crankshaft au camshaft ni nini, sasa ili kuweza kujua muda gani wakati cylinder fulani inafanya kitu gani na inahitaji nini, hizi CAMSHAFT na CRANKSHAFT POSITION SENSOR kuna uchawi unaziwezesha kujua ipi niaje, na kupleka huu umbea kwenye computer ya gari namna tulijaribu kumbushana au kuoneshana🍻

#crankshaftpositionsensor #camshaftpositionsensor #5021tips


ENGINE COOLANT TEMPERATURE SENSOR

Jinsi unavyojua, kifaa chenye uwezo kutembeza umeme kinabadilika kulingana ujoto au ubaridi🤔! So computer ya gari inatuma umeme kuzunguka kwenye hii ENGINE COOLANT TEMPERATURE SENSOR , kuligana ujoto/ubaridi umeme (volts) zitazorudi kwa computer, either itapungua au kubaki niaje namana tulioneshana👨‍🔧


AUTO TRANSMISSION tech & DIAGNOSIS outlines

Kwenye AUTO TRANSMISSION, uchawi zaidi zaidi ni wa valve ambao valve zinategemea solenoid, zingine ni pressure sensor na temperature sensor! SO, kama ulihelewa vizuri kuhusu blaa blaa za hizi sensor kwenye system zingine, then ili muradi picha inakuonesha hii sensor iko wapi, then troubleshooting AUTOMATIC TRANSMISSION troubles ni kama kunywa maji🍻!

#VALVEBODY #AUTOMATICTRANSMISSION #5021tips


TROUBLESHOOTING CONTROL SYSTEMS

Uchawi kuweza blaa blaa ya ma sensor, control boxi, sijui actuators ni kujua mfano ni sensor gani, iko wapi, inafanya kazi gani, inafanyaje hiyo kazi as in iliundwaje (how it is made), nk! So ukipata umbea huu wote ndo utajua inahitaji kupeleka au kutoa umeme gani kutoka wapi au blaa blaa as we explained in here👨🏼‍🎓 !

#electricalcontrolsystems #automotivesensors #5021tips

Translate /Tafsir /Traduire