Electronics Programming (ARDUINO)

Usisome tu upuuzi huu! Fanya na vitendo!
Huko chini, tunaweka sampuli za kufanya mazoezi nazo!
Unahitaji tu kompyuta ya kawaida!

Tafadhali fanya mazoezi ya kutumia hizo zana pepe, yaani zisioshikwa but zinaonekana!
Kufanya mazoezi ili kukushawishi uanze kufanya vya ukweli๐Ÿ˜Ž!
Alafu, hizo vifaa venyewe, unaeza kuzipata popote nchi yeyote uliopo, Ghana, Jamaica, Rwanda, Barboados, Botswana, Trinidad, ayneK๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ, popote ulipo, seen๐Ÿค”?

HAPA UJANJA tu๐Ÿ˜Ž!

Naamini unaona Watu wakawaida wakitengeneza, kuunda vifaa vya ajabu!
So, kwa kutumia mfano wa mradi huu, drone,
wa ndege isiyo na rubani,
yaani, drone, ‘duloni‘ ๐Ÿ˜œ๐Ÿคฃ๐Ÿ˜!
Ndiyo, najua unajua kazi nyingi tofauti zinazofanywa na ndege isiyo na rubani!

Na jinsi inavyofanya kazi ikiruka kote kama ndege!
Kuwa na mtazamo๐Ÿค”!
Katika ‘duloni’, ๐Ÿ‘‡
sehemu kuu ni mota!
yaani, electrical motors, SOZI๐Ÿ‘‡!
Hizi mota zina feni (m) zinazozunguka!
Kama ilivyo๐Ÿ‘‡,
SOZI inadhibiti m!
Uchawi wa drone, jinsi inavyofanya kazi, ni kudhibiti, kuchezea hizo mota zenye mabawa!
Ndani ya drone, hakuna kitu ngumu!
Ndiyo, unajua uchawi wa mota๐Ÿค”!
Umeme ukipungua, kasi pia inapungua!
Kugeuza pande za betri, hubadilisha mwelekeo ambao mota inazunguka!

So, kasi na mwelekeo wake wa mzunguko unaweza kudhibitiwa (controlled) kwa kudhibiti umeme wake!
Mota hizi, SOZI, zinadhibitiwa na kompyuta, Q!
Na kumbuka kompyuta inafanya kazi kulingana na jinsi ilivyoamriwa (ilivyopangwa) programmed kufanya, yaani, how it’s coding is coded๐Ÿคฃ๐Ÿ˜‚ !โ˜Kulingana na ujumbe kutoka kwa kitambuzi, sensor ama controller (A), jinsi unavyotaka drone iende, kompyuta (P) itatuma huu ujumbe kwa kompyuta mwenzake, Q ๐Ÿคทโ€โ™‚๏ธ!
Obviously kwa kupitia utaratibu, B, usiotumia waya!

๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡
Ebu tazama picha hii kwa maakini, ili tujaribu kujadiliana pamoja!
Kumbuka, nilitumia tu drone kama mfano, lakini kuna vifaa vingi sana vinavyotengenezwa kwa kutumia upuuzi huu!
Kwa hivyo, usiweke tu mawazo yako kwenye drone pekee๐Ÿ˜๐Ÿ˜œ!
Sasa, mota hizi๐Ÿ‘‡, SOZI, zinauzwa popote mdukani!
Hata hiyo kompyuta (Q)ย  yaani mazabodiย  (motherboard), inauzwa kila mahali dukani, lakini inauzwa ikiwa tupu, tupu bila amri yoyote, yaaniย  without programmed instructions, ama tuseme data!
Niiga, naamanisha maagizo ya jinsi ya kudhibiti mota, bomboclat๐Ÿ˜๐Ÿคฃ๐Ÿ˜œ!
Hivi ndivyo upuuzi wa ARDUINO unavyokujia!
Kuna kompyuta hizi tupu zinazouzwa kila mahali!
Kompyuta hizi zinajulikana kama ARDUINO,
..yaani
Arduino Development Boards!

Nikisema ‘kompyuta‘ akili yako isiwaze tu ile ya kawaida ambao kila ameaozeoa๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ๐Ÿ˜œ!

Alafu kuna aina nyingi tofauti za hizi, ‘kompyuta’, yaani maza boadi za ANDROID, na zinaweza kugawanywa kulingana na ukubwa wake, madhumuni yake, sehemu zake, na mengi zaidi!

Na kama unavyojua, kwamba kompyuta hufanya kazi kwa kutoa matokeo kulingana na ingizo!
Kama unavyoona kwenye hii picha๐Ÿ‘‡ hapa chini,
kompyuta (B) ilipangwa kusikiliza kitambuzi (A)!


Mradi tu kitambuzi (A) kinatuma ujumbe kuhusu uwepo wa pombe (P) kompyuta (B) huambia kiendeshaji (C) kufungua mlango.

Vitambuzi(A) โ˜, yaani sensa (sensor) kama (A)โ˜zinauzwa kila mahali!
Unapoendelea kufikiria nini cha kuunda, kutengeneza, insha’Allah,
unaweza kutaka kutumia takataka hii,
BONYEZA HAPA

..kujifunza kuhusu vitambuzi tofauti
,
jinsi vinavyotumika katika hali halisi ya maisha, kwenye vifaa fulani vya kielektroniki!
CLICK HERE get an idea of how what where sensors applied!
Actuators (C) viendeshaji, vinauzwa kila mahali!Ndiyo, na tena๐Ÿคช,
Unapoendelea kufikiria nini cha kuunda, kutengeneza, insha’Allah,
unaweza kutaka kutumia takataka hii,
BONYEZA HAPA

..kujifunza kuhusu viendeshaji tofauti
,
jinsi vinavyotumika katika hali halisi ya maisha, kwenye vifaa fulani vya kielektroniki!

CLICK HERE not to get ideas of how what where sensors applied, bomboclat๐Ÿคฃ๐Ÿ˜œ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜!
Kumbuka, nikisema ‘kompyuta‘ (B), akili yako isiwaze tu ile ya kawaida, akina laptop, ambao kila ameaozeoa๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ๐Ÿ˜œ!So ata kompyuta(B) โ˜, yaani ‘maza bodi‘ kama (B)โ˜zinauzwa kila mahali!Kompyuta huja ikiwa tupu, bikira!
Hapa ndipo unapoweka programu, maelekezo (data)!
Wale wa www.arduino.cc ย wanaotengeneza kompyuta hizi, hufanya hivyo kwa hiari, voluntarily๐Ÿค!
click here download
Programuโ˜ unayohitaji kuandika maelekezo (uchawi) katika ‘maza bodi’ kompyuta hii, ni bure, wala bila masherati ya “just 2 beers“๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜๐Ÿ˜œ!
Bofya hapa kuipakua!
Juu ya kuandika (coding) huo uchawi,
tafadhali usiogope! Usikaate taama!
Niiiga, usipoteze matumaini ya kuwa mbunifu!
Kumbuka, HAPA UJANJA tu๐Ÿค , mtu yeyote,
ikiwa ni pamoja na Wewe,
unaweza kuwa mjanja, kufanya chochote, mwenyewe, peke yako, insha’Allah!
Be confident๐Ÿ˜Ž!
Kwa mfano;
Ukitaka kubuni uchawi,
๐Ÿ‘‡
..wa kutenganisha, kutoa chupa za bia katika chupa zinaopita!Sasa, unaanza kufikiria kuhusu unachotaka kudhibiti, yaani ku controll๐Ÿค”!
Unaweza kugundua kuwa chupa ya pombe ni nyeusi! Kitu kingine kinaweza kisiwe cheusi, bila giza kama chupa!Labda kwa sababu ulibofya hapa, na una wazo la vitambuzi tofauti!
Sasa unafikiria, na unapata kitambuzi kinachoweza kugundua vitu namna hivi kwa njia ya kipekee!Huenda ikawa ni kwa sababu, chupa ya pombe ni nyeusi, inafanya uchawi tofauti, kwa chochote ambacho hii (sensor), yaani kihisi hiki, hutumia kuhisi๐Ÿคทโ€โ™‚๏ธ.
Naaam, insha’Allah, tena, huenda ikawa ni kwa sababu, chupa aina zingine , sio nyeusi, zinafanya uchawi tofauti, kwa chochote ambacho hii (sensor), yaani kihisi hiki, hutumia kuhisi๐Ÿคทโ€โ™‚๏ธ.Sasa, katika huu mradi wako wa kutengenisha, unaona jinsi sehemu ya kuhisi (sensing) tayari imeshughulikiwa๐Ÿค”?!
Upande wa kitambuzi (A) ni tayari, umeweza kupata kitambuzi, sensor ya kuchunguza hizo chupa!
๐Ÿ˜๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ Sasa usifikirie kukata mkono wa mtu, eti utumike kama kinendeshajiย  (actuator)kutoa au kusukuma chupa ya pombe iliyogunduliwa!
Kuna viendeshi vingi sana, yaaani vipengele vya umeme, unavyoweza kufikiria!
Inaweza kuwa mota inayozunguka, au kitu kingine chochote, kama solenoid inayoweza kuvuta au kusukuma chupa ya pombe iliyogunduliwa๐Ÿ‘Œ!
Sasa, ni masha’Allah, kitambuzi (A) tayari!
Kiendeshaji (C) nacho tayari!
Kwenye kompyuta(C) ndo mchwi mwenyewe๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ๐Ÿ˜!
Nakukumbusha, usiogope uchawi wa programming, coding ya kompyuta!
Hebu tuendelee polepole, tunapogundua jinsi ya kupata uchawi, coding maagizo ambayo kompyuta (B) inapaswa kufanya kazi nayo!
Kwanza kabisa, hii ‘zig zag’ haina uhusiano wowote na EEPROM work!
Huhitaji (sio lazima)ujuzi wa kujua jinsi ya kusoma, kubadilisha (edit) au kuandika, data kwenye EEPROM!
Lakini, hata kama unataka kujifundisha mwenyewe, EEPROM work, obviously HAPA UJANJA tu๐Ÿค !
Click here, jifunze mwenyewe, jazka’Allah๐Ÿคฃ๐Ÿ˜‚

Kwanza, tukubali ukweli huu๐Ÿค”!

Huwezi kuamka tu na kuanza kuandika amri (programu) hizi instructions ambazo kompyuta hutumia๐Ÿคช!
SI kwamba huwezi, lakini inachukua muda, wakati kumbe huhitaji maandalizi yoyote ili kuunganisha vitambuzi na viendeshaji, kwenye kompyuta (maza bodi)๐Ÿคทโ€โ™€๏ธ!
Ili kusaidiana, mwanzoni, upande wa programming, wewe zingatia tu kujua jinsi ya kuunganisha kebo ya usb kwenye kompyuta yoyote ya kawaida!
Kama vile unavyoweza kuhamishia picha, muziki kwenye fulashi diski (flash disc), hamishia programu (coding) ambayo Suzan atakutumia, kulingana na mradi uliowaomba wakubunie!
Na lazima ujue, kuunganisha tu waya ya USB na kuhamishia purogram, sio kua mjanja๐Ÿค!
Kwasababu bado unatutegemea kuandikia, kuundia purogramu!
Ndo maana tunatendelea taratibu wakati tunapeana uchawi wa wewe kuweza kujiuundia programu mwenyewe, inshaรllah๐Ÿคž!

A) Tumetambua kwamba kila aina sensors vitambuzi (A)ย  vinapatikana madukani, na ni rahisi kuinganisha kwenye (B) kompyuta (maza bodi)!
C) Tumetambua kwamba kila aina ya actuators viendeshaji (C) vinapatikana madukani, na ni rahisi kuinganisha kwenye (B) kompyuta (maza bodi)!
B) Tumetambua kwamba unaeza kupata, ata kama mwenyewe bado hujajua uchawi wa kuunda (B) purogramu (coding), yaani kuandika maelekezo jinsi kompyuta itaunganisha vitambuzi (A) kwa viendeshaji (C)!
Na ukumbuke hizi kompyuta (B), yaani maza bodi zipo aina tofauti, lakini utoafuti wazo ni mdogo tu!
insha’Allah, polepole polepole, tunaendelea kujadili kila sehemu iliyo kwenye maza bodi hizi, ili usifanye makosa yoyote, jazak’Allah๐Ÿคž!


Tunaenda polepole, tunapokumbushana kwa undani, kuhusu uchawi wote, kuanzia misingi ya kuhamisha programu kutoka kwa kompyuta ya kawaida, hadi kwenye kompyuta fulani, chipu(Z) EEPROM!Tutajadili kwa undani, kila sehemu, kila kitu kwenye kompyuta hii, maza bodi!
Huna haja ya elimu yoyote ya shule!

HAPA UJANJA tu๐Ÿป


Part-0
Kuweka data (maelekezo) kwenye maza bodi (Arduino board)

Software ya kusaidia ‘kopi & pesti‘ย  kuhamisha programu iende kwenye kompyuta EEPROM, Z, inapatikana popote!
Na tayari uko nayo!
click here download
Tuseme๐Ÿค”, kwaย  kulingana maagizo uliyotoa๐Ÿ˜Ž!
Sasa umepewa na una data, ambayo inalingana na jinsi ulivyopanga vitambuzi na viendeshaji, kwenyeย  maza bodi๐Ÿง!
Mfano wa maelekezo coding data
Na ukumbuke hizi kompyuta (B), yaani maza bodi zipo aina tofauti, lakini hata kama utofauti wazo ni mdogo tu!
So, kwenye programu๐Ÿ’ป, kwa kutumia kompyuta ya kawaida, yaani laputopu๐Ÿ’ป,
hakikisha umechaguaย  ‘maza bodi’ ya Arduino sahihi, halisi, yenyewe unaotumia๐Ÿ‘Œ!
Kwenye kompyuta ya kawaida๐Ÿ’ป, kama vile jinsi unavyoweza kutafuta video, muziki, kutoka mahali ulipoihifadhi, sasa tafuta data hiyo ambayo SUZAN alikutumia! Data ikifunguliwa, insha’Allah, unaweza kuangalia, kutazama, kufuata maagizo wakati unajifunza, unafuatilia jinsi uchawi unavyofuata!
Tafadhali ๐Ÿ™usibadilishe chochote,
bofya tu kitufe kimoja tu, UPLOAD, ili kupakia, kuandika au kutuma data kwenye ‘maza bodi‘๐Ÿค!Ukibadili bila kuelewa unachobadilisha,
tayari umeharibu kila kitu!
So hapo lazima utume vinywaji vingine, Suzan akushugulikiye na ujanja kwa debugging!

Part-1

Kuweka, ama kutumia kebo ya usb kuiunganisha kompyuta kwa ๐Ÿงna maza bodi (Arduino board)
Si sahihi kuamuru, kuamini, kwamba ni aina moja tu ya kebo inayotumika๐Ÿ‘Œ!
Insha’Allah, tumia kebo inayofaa kwa tundu lolote la USB utakalopata๐Ÿ˜Ž!

Kumbuka๐Ÿค”, kuna upuuzi mwingi tofauti ambao unaweza kusababisha kebo kutokuwa na maana๐Ÿšฝ!
Click Bonyeza Hapa
Hapaโ˜ tulijaribu kujadili kila upuuzi kuhusu kebo hizi๐Ÿคทโ€โ™€๏ธ!

Part-2

Hongera๐Ÿคž!
Umefanikiwa (na kwa usahihi) kuunganisha kebo ya USB!
Kwa ufahamu wako tu, ujue kwamba,
data kutoka USB, haiendi moja kwa moja kwenye chip, microController (Z)๐Ÿ˜Ž!
Kuna kitu (X) kama EEPROM (IC, chip) Driver ama microController๐Ÿค!
ย Whatever, but kifaa (X) ni cha kutafsiri,
kuunganisha data yote inayotumwa kupitia USB,
ili iwe na maana kwa moduli (Y)๐Ÿง!
Kumbuka kutoweka tu ubongo wako kuganda kwenye kifaa kimoja maalum๐Ÿ‘Œ!
Inaweza kuwa tofauti, ATmega16U2, ama ATmega32U4 ama FTDI FT232RL ama CH340G, yeyote, insha’Allah, kulingana aina ya module๐Ÿง! Ujanja ni kujua tu kwamba kuna kitu (Y) cha utendaji huu!
Yaaani, daima kuna kitu kama EEPROM (IC, chip) Driver ama microController, kifaa cha kutafsiri, kuunganisha data yote inayotumwa kupitia USB!
By the way, ukitaka ule ujinga kugundua, upimaji, taka taka yote jinsi vidude mbali mbali kwenye maza bodi, pamoja na jinsi vinafanya kazi,
usibonyeze HAPA, but click here!

HAPA UJANJA tu๐Ÿคž

Part-3

Masha’Allah๐Ÿคž!
Tumefanikiwa (na kwa usahihi) kuandika data, instructions maelekezo kwenye chip (Z)!
Kwa ufahamu wako tu, ujue kwamba,
leo, mwaka 1990 wakati tunaandika taka-taka hizi, Arduino nyingi zinatumia microController (Z)๐Ÿ˜Ž!

Sio kwamba hakuna,
Arduino za microPROCESSOR๐Ÿ˜œ!

Bonyeza Hapa ukitaka kutofautisha microPROCESSOR kwa/na microCONTROLLER๐Ÿง!
Lakini, tafadhali๐Ÿ‘Œ, fahamu kwamba kuna uchawi wenye microPROCESSOR (Q)๐Ÿ˜Ž!

Naaam, microCONTROLLER (Y), hizi vitu ni vingi,
aina tofauti na vyenye sifa tofauti!
Maana yake unapaswa kuwa mwangalifu jinsi unavyochagua
๐Ÿง!
kwa mfano, kuna…

ATmega328P๐Ÿ˜ŽKumbuka “vitu hivi” vinaweza kuja katika aina mbili, DIP (s) au SMD (z) ๐Ÿคทโ€โ™‚๏ธVyote uchawi ni sawa, na vitafanya kazi kwa njia ile ile.
Tofauti pekee ni kwamba chipu ya DIP (s) ni inayoweza kutolewa hukuruhusu kubadilisha, kukiwepo vurugu yeyote!

ATmega328๐Ÿ˜Ž
Ndiyo, hizi vitu (Arduino) zina ukubwa tofauti!
Leo mwaka huu 1990 wakati tunaandika ujinga huu, ilikuwa Arduino Nano mojawapo ya mbao ndogo, ikiwa karibu nusu ya ukubwa wa Uno๐Ÿ‘Œ!

Arduino MKR’s ๐Ÿ˜Ž
Baadhi ya hizi vitu, huja namna fulani, kuzingatia sana kazi maalum!
Kwa mfano, hii Arduino MKR Zero ni bodi nzuri kwa miradi mbalimbali ya muziki. Inakuja na hiyo chip, SAMD21 Cortex-M0 inajulikana kwa kula, kutumia umeme kidogo๐Ÿ‘Œ!
Arduino MKR Zero in sehemu ya SD card pamoja na vipengele vingine SPI (S,O,Z)๐Ÿคช!
Ndiyo, kumbuka, baadhi ya hizi vitu, huja namna fulani, kuzingatia sana kazi maalum!
Mfano mwingine ni waย  Arduino MKR WiFi 1010 ikiwa unataka uchawi wa IOT (Internet Of Things)
Ina vifaa sipecio (S,O,Z) kwa muunganisho wa WiFi na Bluetooth๐Ÿ“Œ!
Kuna MKR Vidor 4000 yenye FPGA processor pamoja na controller ya Intel Cyclone 10CL016, SAMD21 Cortex-M0+ …
Unaona hiyo NINIAW102 module, LiPo ya battery, Micro HDMI, MiniPCI Express, MIPI Camera connector, na vipengele vingine vya SPI connectors.

 


Bodi hizi zipo nyingi na tofauti siwezi kuzimalizia zote๐Ÿ˜‚๐Ÿคฃ๐Ÿ˜‚
Acha nisikusisimue kwanza๐Ÿ˜œ!
Hebu tutumie ubao ๐Ÿ‘‡wetu rahisi tunapokumbushana, polepole polepole๐Ÿง!

Part-4

Hii kitu kinahitaji umeme ili ufanye kazi,
kwa hivyo upumbavu huu unajumuisha ujinga wote wa jinsi tunavyoweza kuipatia umeme, bodi๐Ÿง!
Kama unavyojua tayari๐Ÿค ,
bodi hizi ni nyingi, na tofauti๐Ÿ‘Œ!
Kila, inaweza kutumia nguvu tofauti ya umeme๐Ÿ˜ฒ!
Kwa hivyo,
ni ‘ujanja’ kwanza kujua mahitaji ya umeme ya bodi hiyo unayoshughulika nayo๐Ÿ‘Œ!
Kuna namna tofauti,
kama(S,O,Z,I)๐Ÿ‘‡
za kusambaza umeme kwenye bodi,
ikiwa ni pamoja na “sheria na masharti” ya kila njia๐Ÿคช!
Njia rahisi ni kwa kupitia USB,
ambao hutoa 5V kutoka kwa mfano,
kompyuta, ‘pawa benki‘, adapta ya ukutani, nk๐Ÿง!
Kuwa tayari, bodi inaweza kutumia kebo/soketi yoyote ya USB isiyo rasmi๐Ÿคทโ€โ™€๏ธ!
(I) Ujue kwamba volteji ya USB ni 5V,
pamoja na kupungua nguvu juu ya kusambaziwa katiaka kila mahali๐Ÿ˜ข!
Je๐Ÿค”, ikiwa uchawi wako unahitaji umeme wa ziada?
Masha’AllahโœŒ, kuna mahali pa kuingiza kebo yenye umeme kutoka ๐Ÿ”Œkwa usambazaji wowote๐Ÿง˜โ€โ™‚๏ธ!
Inaeza ikawa battery yenye kati ya, 8V na 12V๐Ÿคทโ€โ™€๏ธ!Inaeza ikawa ile adaputa ya kuchomeka ukutani kwa umeme wa nyumbani๐Ÿคทโ€โ™€๏ธ!
Adaputa (S) inapaswa kuweza kubadilisha umeme kuwa (O) kati ya 9V, na 12V๐Ÿฅ‚!
..vinginevyo usumbufu fulani unaweza kusababishwa
Ikiwa, kwa makosa, utabadilisha mwelekeo sahihi wa kebo, kwa(M) kuna uchawi fulani unaoweza kukidhi ujinga wako๐Ÿงปuende๐Ÿšฝ!
Lakini, assume, fikiria haipo, kuwa mwangalifu tu๐Ÿ˜Ž!
Ubongo wa bodi unahitaji umeme mdogo,
kwa hivyo mfumo huu (I) husaidia kudhibiti, kurekebisha, umeme wowote unaoingia๐Ÿšง!Tuseme, huna kebo (O, Z) ya kuingiza kwa (C)๐Ÿ˜ข!
Katika (I) kuna mahali pa kuunganisha waya,
ikiwa zina๐Ÿš‘,
umeme uleule ambao ungeingia katika
(C)!Katika (S), uchawi ni kwamba, mradi tu umeme utagunduliwa katika (I), hata kama USB imeunganishwa, umeme wake (S) utapuuzwa,
badala ya umeme katika (I) “shikamoo“๐Ÿ˜œ!
Inaweza kuwa kwa sababu yoyote๐Ÿคทโ€โ™€๏ธ,
inaweza kuwa (M) imeharibika au chochote kile๐Ÿš‘!
Kwa (Q) unaweza kusambaza moja kwa moja umeme mdogo wa 3v na au 5V๐Ÿ˜ฒ!
Kumbuka, ikiwa usambazaji mwingi wa umeme umeunganishwa, uchawi wa bodi unaweza kuchagua kiotomatiki usambazaji bora wa umeme, ukipendelea ule wenye volteji ya juu๐Ÿ˜Ž!
By the way, ukitaka ule ujinga kugundua, upimaji, taka taka yote jinsi vidude mbali mbali kwenye maza bodi, pamoja na jinsi vinafanya kazi,
usibonyeze HAPA, but click here!

Part-5

Alafu…..


Sasa, nimechoka kuandika๐Ÿ˜ข!
Utakuwa unarudi hapa kuangalia,
kila baada ya sekunde 43,200!
Utapata kitu kipya zaidi, insha’Allah๐Ÿคž
Bonyeza hapa, mwambie mhudumu, ni mimi ameketi hapa pembeni๐Ÿ˜Ž!

May be whatever is causing You believe MUST do some nonsenseย to the vehicle, is some minor external problem with the sensors or actuators๐Ÿคทโ€โ™‚๏ธ!
So, this ujanja is how to check, verify all the control electronics in the vehicle, are in proper order!
click here

๐Ÿ‘‡
IMMO OFF files
โ˜โ˜
click
These files to disable immobilizer system so the ecu accepts any random key used!

HAPA UJANJAtu, hii ndio jinsi ya kugundua, kupata na kupima componets za ECU, kisha suluhisha shida hiyo. inshaAllah๐Ÿ‘‡
Click Here
bonyeza HAPAย 

ECU cloning, duplicating or switching memory data’s,
flash memory data, EEPROM memory data, jogolize data,
HAPA UJANJA tu!
click HERE

WinOLS ni programu yenye uchawi wa kuwezesha kubadilisha, kurekebisha data iliyomo kwenye ย ECU.
Ina maana unaeza kutoa/kuzima hizo mifumo zenye usumbufu kwenye gari, zikiwemo IMMOBILISER (kufanya immo off). kutoa DPF, EGR, ADblue, kubadili TURBO zenye umeme, yaaani inafanya kazi nyingi kama ECU tuning, uamuzi ni wako tu๐Ÿคทโ€โ™‚๏ธ!
Click HERE

Ujanja wa EEPROM work ni muhimu, ukitaka kumbuka niaje,
…bonyeza HAPA UJANJA tuย 


Translate /Tafsir /Traduire